Jinsi ya kufikisha kuku 1000 wa asili ndani ya muda mfupi

Wangari Maathai nimekuita hapa
 
Najifunza hapa kama mfugaji mtarajiwa.
 
Nashukuru kwa mada nzuri ila nisaidie zaidi hapo kwenye kuweka mayai yasiyo ya jogoo...je siku unaweka mayai ya jogoo inakuwaje
 
Nashukuru kwa mada nzuri ila nisaidie zaidi hapo kwenye kuweka mayai yasiyo ya jogoo...je siku unaweka mayai ya jogoo inakuwaje
Ndugu hapo unakuta mfugaji anataka kuku wote watotoe vifaranga kwa wakati mmoja ili iwe rahisi kuwapa hata chanjo.

Lakini kuku hutofautiana muda wa kutaga na kutotoa pia sasa ili waende sawa, wale kuku wanaowahi kutaga na kuanza kaatamia wanawekewa mayai mabovu au yasio na mbegu/kisasa ili yule kuku aendelee kupoteza nayo muda huku akisuburi wengine.

Ikifika muda kuku hata 13 wameanza kulalia ndio unachukua yale mayai mazuri unawawekea kwa pamoja
 
Niliwapa chanjo zote lakini mdondo/kideri ulivyoingia tu nikakuta kuku wote 200 wapo chini😎😎😎
Sijakata tamaa nataka niagize tabora kuku 300 wa miezi 5
Umanunua kwa bei gani huko Tabora.
 
Asante kwa majibu. Wewe unauza au inabidi kwenda minadani
Hapana Mimi siuzi ila nilikuwa nanunua kuku wenye miezi 5 nakuja kuwafuga mwenyewe,nilisitisha ufugaji kwa muda ila kwa sasa nataka nirudi tena
NB:Mimi kuku nilikuwa sinunui mnadani nilikuwa nanunua vijijini,ila ukitaka kununua mnadani kuwa makini kuku wengi wanakuwa wagonjwa na epuka kununua kuku kipindi cha kiangazi kwa sababu kipindi cha kiangazi magonjwa mengi yanashamiri
 
Asante kwa taarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…