Jinsi ya kufunga siku 52 kwa Kila mwaka kirahisi kwa afya

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!!

Naamini Kila mtu anajua ya kuwa, chakula ni muhimu Kwa ajili ya AFYA ya MWILI, lakini pia, matabibu wamethibitisha kuwa chakula pia ni chanzo Cha magonjwa mengi tu yanayosumbua watu wengi tangu zamani.

Wiki Moja, Ina siku Saba, ukitenga siku moja iwe special Kwa ajili ya KUFUNGA, kuupumzisha mwili kusaga chakula, uwe na HAKIKA utakuwa umepata siku 52 Kwa mwaka mzima za kufunga na kuupumzisha mwili wako Ili uwe mwenye AFYA zaidi.

Na ufungaji huu, usiwe Ule wa kupania, wa kuamka usiku kula, HAPANA, ukishakula chakula Cha usiku saa mbili au saa tatu, ukimaliza kufanya Sala ya usiku, nenda kalale saa nne au saa Tano usiku, Kisha ukiamka asubuhi, endelea na KUFUNGA Hadi sasa kumi na mbili ya jioni Kila wiki. Saa nne usiku Hadi sasa 12 jioni, hayo ni masaa 20. Na Kwa kushauri, siku ya Saba ndio siku special ya KUFUNGA na kuomba na kufanya Ibada hiyo special.

ZIFUATAZO NI FAIDA ZA KUFUNGA.

Faida hizi zinapatikana katika KITABU Cha (Isaya 58:1-14).

1. KUFUNGUA VIFUNGO VYA UOVU.

Kufunga, ni kufungua VIFUNGO VYA UOVU, ikiwa ulifungwa Uchumi, AFYA kichawi, kufungua VIFUNGO hivyo ni KUFUNGA.

2. AFYA YAKO ITATOKEA MARA.

Kufunga, kunaleta AFYA ya MWILI maana Tendo Hilo hupumzisha mifumo ya umengenyaju chakula, pia husaidia kuchoma mafuta mwilini nk nk.

3. KUWAFUNGUA WALIOFUNGWA.

Kufunga na kuomba, kunasaidia wengi WALIOFUNGWA katika vifungo mbalimbali kimwili na kiroho wapate KUFUNGULIWA.

4. KUFUNGUA MILANGO YA KUWALETA WALIOPOTEA NYUMBANI MWA BWANA.

Kufunga, husaidia wote WALIOFUNGWA, wote Walio dhambini wapate kibali kumjua Mungu, wengi wameokoka bila hata kupanga kufanya hivyo sababu ya maombi ya wanaofunga.

5. MAOMBI YAKO YATAJIBIWA KIRAHISI.

Imeandikwa, Mungu Huwa hajibu maombi ya wenye dhambi, maombi ya KUFUNGA,huambatana na TOBA, hivyo ni Rahisi sana maombi Yako kujibiwa ikiwa utafunga.

6. UTAPATA PESA ZA KUGAWIA MASKINI.

Pesa ambayo huzitumia Kwa siku hiyo Moja uliyoitenga KUFUNGA na kuomba, ikitunzwa, ni Rahisi kuitoa Kwa maskini kama sadaka Yako.

7. UTAACHA URITHI KWA VIZAZI VINGI.

Ikiwa umezaliwa familia maskini ambapo hujapata chochote kama URITHI Toka Kwa Babu au baba, utakapoanza Ibada ya KUFUNGA, Mungu atakufungulia milango ya Kupata Mali ambazo utawarithisha watoto Hadi wajukuu, simply, utabarikiwa.

8. UTASTAWI. (Isaya 58:11)

"Naye BWANA atakuongoza daima,ataishibisha NAFSI Yako Mahali pasipokuwa na maji, na kupitia nguvu mifupa Yako, nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui."

Hii inamaanisha kuwa, utapokea wageni, watakula na kusaza nawe hutapungukiwa, Kila ufanyacho, kitabarikiwa na kuongezeka bila kupunguka.

HITIMISHO
Siku SITA, kula chakula chako, siku ya Saba utumie na utoe sadaka kama siku maalum ya KUFUNGA Ili kujilisha Roho Yako chakula na kujiweka karibu zaidi na Mungu. Na njia hii, utaweza KUFUNGA siku 52 Kwa mwaka kirahisi kabisa.

Mungu awabariki.

Ikiwa hujampa Yesu Kristo maisha Yako, fuatisha Sala ifuatayo;

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. Amen

Karibuni 🙏
 
Sisi waislamu tuna ile sunna ya kufunga siku ya juma 3 na Alhmc...pia ipo funga ya nabii daudi hii unafunga siku moja unaacha sku moja....

Naunga mkono hoja...
 
Hiyo ni Kila wiki?
 
Salaam, Shalom!!!

Naamini Kila mtu anajua ya kuwa, chakula ni muhimu Kwa ajili ya AFYA ya MWILI, lakini pia, matabibu wamethibitisha kuwa chakula pia ni chanzo Cha magonjwa mengi tu yanayosumbua watu wengi tangu zamani.

Wiki Moja, Ina siku Saba, ukitenga siku moja iwe special Kwa ajili ya KUFUNGA, kuupumzisha mwili kusaga chakula, uwe na HAKIKA utakuwa umepata siku 52 Kwa mwaka mzima za kufunga na kuupumzisha mwili wako Ili uwe mwenye AFYA zaidi.

Na ufungaji huu, usiwe Ule wa kupania, wa kuamka usiku kula, HAPANA, ukishakula chakula Cha usiku saa mbili au saa tatu, ukimaliza kufanya Sala ya usiku, nenda kalale saa nne au saa Tano usiku, Kisha ukiamka asubuhi, endelea na KUFUNGA Hadi sasa kumi na mbili ya jioni Kila wiki. Saa nne usiku Hadi sasa 12 jioni, hayo ni masaa 20. Na Kwa kushauri, siku ya Saba ndio siku special ya KUFUNGA na kuomba na kufanya Ibada hiyo special.

ZIFUATAZO NI FAIDA ZA KUFUNGA.

Faida hizi zinapatikana katika KITABU Cha (Isaya 58:1-14).

1. KUFUNGUA VIFUNGO VYA UOVU.

Kufunga, ni kufungua VIFUNGO VYA UOVU, ikiwa ulifungwa Uchumi, AFYA kichawi, kufungua VIFUNGO hivyo ni KUFUNGA.

2. AFYA YAKO ITATOKEA MARA.

Kufunga, kunaleta AFYA ya MWILI maana Tendo Hilo hupumzisha mifumo ya umengenyaju chakula, pia husaidia kuchoma mafuta mwilini nk nk.

3. KUWAFUNGUA WALIOFUNGWA.

Kufunga na kuomba, kunasaidia wengi WALIOFUNGWA katika vifungo mbalimbali kimwili na kiroho wapate KUFUNGULIWA.

4. KUFUNGUA MILANGO YA KUWALETA WALIOPOTEA NYUMBANI MWA BWANA.

Kufunga, husaidia wote WALIOFUNGWA, wote Walio dhambini wapate kibali kumjua Mungu, wengi wameokoka bila hata kupanga kufanya hivyo sababu ya maombi ya wanaofunga.

5. MAOMBI YAKO YATAJIBIWA KIRAHISI.

Imeandikwa, Mungu Huwa hajibu maombi ya wenye dhambi, maombi ya KUFUNGA,huambatana na TOBA, hivyo ni Rahisi sana maombi Yako kujibiwa ikiwa utafunga.

6. UTAPATA PESA ZA KUGAWIA MASKINI.

Pesa ambayo huzitumia Kwa siku hiyo Moja uliyoitenga KUFUNGA na kuomba, ikitunzwa, ni Rahisi kuitoa Kwa maskini kama sadaka Yako.

7. UTAACHA URITHI KWA VIZAZI VINGI.

Ikiwa umezaliwa familia maskini ambapo hujapata chochote kama URITHI Toka Kwa Babu au baba, utakapoanza Ibada ya KUFUNGA, Mungu atakufungulia milango ya Kupata Mali ambazo utawarithisha watoto Hadi wajukuu, simply, utabarikiwa.

8. UTASTAWI. (Isaya 58:11)

"Naye BWANA atakuongoza daima,ataishibisha NAFSI Yako Mahali pasipokuwa na maji, na kupitia nguvu mifupa Yako, nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui."

Hii inamaanisha kuwa, utapokea wageni, watakula na kusaza nawe hutapungukiwa, Kila ufanyacho, kitabarikiwa na kuongezeka bila kupunguka.

HITIMISHO
Siku SITA, kula chakula chako, siku ya Saba utumie na utoe sadaka kama siku maalum ya KUFUNGA Ili kujilisha Roho Yako chakula na kujiweka karibu zaidi na Mungu. Na njia hii, utaweza KUFUNGA siku 52 kirahisi kabisa.

Mungu awabariki.
umeongea jambo la maana sana, ila tu ufanye hivyo ukiwa makini usije kuwa unafunga kimazoea na kuomba huombi, matokeo yake ukawa umesusa tu kula. but all in all, maombi ya kufunga siku zote hayajawahi kukosa matokeo. mtu mwombaji wa kufunga ni tofauti kabisa na mwombaji wa kawaida. kwasababu unapofunga unaushusha mwili (humble yourself before God) na ukishuka Mungu anakuinua, Mungu anakusogelea zaidi. kuna sheria moja inaitwa:

1. soma sana Neno Utamjua sana Mungu. ukiliweka Neno la Mungu moyoni umemweka Mungu moyoni. lina uvuvio lazima utaona utofauti tu.

2. Mtafute sana Mungu kwa kufunga na kuomba nawe utamwona. unapoomba sana unakaribisha uwepo wa Mungu, na uwepo wa Mungu manake ni Mungu mwenyewe, uchafu wote wa shetani kama magonjwa, mikosi, mitego yote n.k vitakimbia vyenyewe.

3. the more unavyomsogelea Mungu the more anakuwa karibu nawe, the more unavokuwa mbali naye the more anakuwa mbali nawe.
 
Back
Top Bottom