Samedi Amba LLC
Member
- Apr 5, 2024
- 81
- 117
Habari wanajamvi,
Natumaini Krismasi inaenda vizuri. kwa mliowahi kanisani, hongereni. Kwa wengine ambao wanatumia fursa hii kupumzika, nawatakia mapumziko mema (binafsi likizo ya wiki moja itaanza jioni ya leo. Krismasi kwangu ni fursa ya kuwasaidia wahitaji).
Leo nlikuwa mtandaoni, nikaona makala moja ya the Citizen inayoashiria mabadiliko fulani katika usafiri nchini Tanzania. Hii inahusu sana ruti ya Dar-Dodoma, ambayo kwa muda mrefu mabasi walitumia kujipatia faida.
Tangu SGR kuanza mwendo, ni kweli kuwa ruti hii hailipi tena kama zamani. Takwimu nlizopata katika gazeti hilo ndo hizi hapa:
- Shabiby wamekiri kuwa biashara imebadilika. Wamelazimika kukatisha safari za saa 9 na saa 11 asubuhi. Wamegundua kuwa abiria hawakati tiketi mapema kama walivyokuwa wakifanya zamani.
- Kimbinyiko wamesema kuwa wamelazimila kupunguza magari ya Dar-Dodoma, kutoka mabasi 10 hadi 4.
- Basi la ABC limelazimika kutazama upya utoaji huduma, kwa kuwa walikuwa wakitegemea ruti ya dar-dodoma mno (nilikuwa shabiki mkubwa wa basi la ABC upper class)
- TABOA (Tanzania Bus Owners Association) wametoa tamko kuwa mabadiliko ni dhahiri, na kuwa "SGR imeathiri utendakazi wetu kuliko tulivyotegemea hapo awali."
- LATRA wamegundua pia, kupitia takwimu zao, kuwa idadi ya wasafiri na mabasi katika ruti za Dar-Dodoma zimepungua tangu SGR kuanza kazi.
Mabadiliko
Mabasi yakaamua yafutayo ili kukabiliana na mazingira:
- Shabiby wameagiza mabasi 30 mapya, ili kuwawezesha kufikia ruti ambazo SGR haifikii, km Dom-mwanza, Dom-Kigoma na Dom-Arusha. Wameamua kutanua muda na kutoa usafiri muda wa saa 2 , saa 3 na saa 5 usiku.
- Kimbinyiko wameamua kufungua ruti 6, ikiwemo Dar-Tunduma, Dar-Arusha, Dar-Moshi na Dom-Arusha. Wanapanga kuelekea Nairobi kuanzia 2025.
- LATRA wana mpango wa kukutana na wamiliki wa mabasi ili kuoanisha huduma za SGR na mabasi, hasa katika vituo vya SGR.
Cha Kujifunza
Katika maisha na biashara, ni rahisi kukariri "njia za zamani". Labda ni mazingira fulani tulozoea. Au fursa na eneo fulani la kazi. Au hata kikundi fulani cha watu tuliokuwa tukiwadumia kwa muda mrefu.
Lakini mabadiliko huja, na mara nyingi mazingira ya mabadiliko huwa nje ya tunachoweza kucontrol. Cha kufanya: badilika na mabadiliko.
Watu wengi huanza kupingana na kupigana na mabadiliko. Lakini mbona tuumize mkono kujaribu kubamiza ukuta wenye rafu?
Wenye mabasi wameamua kubadilika. Tubadilike na sisi.