Jinsi ya kuifanya gari yako itumie mafuta vizuri zaidi kuliko ulivyozoea

Wakuu naomba kujua kuna madhara gani kutembelea gari ambayo ina ball joints zilizochoka (zinatoa mlio kama vigololi vinagongagonga) maana kwasasa mfuko hauko vizuri, na gharama zake za replacement zikoje kwa Spacio new model.
Ball joint nina uhakika mbili hazitazidi 40K, ukiwa na 50K unamaliza tatizo. Hio ndio raha ya Toyota mkuu hili chama ni burudani esp. ukiwa unamiliki gari jamii ya corrolla.
 
Hiyo namba 6(mfuniko wa tank la Petroli) unaweza shangaa tu sensors za ABS, CHECK ENGINE na CHECK VSC zinawaka ukabadili kila kitu haswa kama unatengeza kwa mafundi wapiga ramli na zisizime.. Ukicheck mfuniko unakuta uko loose ukizima na gari na kuufunga mfuniko vizuri kila kitu kinakaa sawa… ukinunua used inabidi kubahatisha sana ambao unaendana haswa na gari yako…
 
Kuna mafundi/wauzaji wanatuambia tuweke 20W 50 kama kilometer zimezidi 150k hata kama manufacturer ame recommend 5w30, hili unalizungumziaje?
 
Kuna mafundi/wauzaji wanatuambia tuweke 20W 50 kama kilometer zimezidi 150k hata kama manufacturer ame recommend 5w30, hili unalizungumziaje?
Swali zuri
Nakutana na huo ushauri mara kwa mara.

Na mimi nasubiri jibu
 
Kuna mafundi/wauzaji wanatuambia tuweke 20W 50 kama kilometer zimezidi 150k hata kama manufacturer ame recommend 5w30, hili unalizungumziaje?
Hakuna fundi anayeelewa gari kuliko manufacturer.
Fuata maelekezo ya manufacturer
 
 
Hakuna fundi anayeelewa gari kuliko manufacturer.
Fuata maelekezo ya manufacturer
Usiukwepe uhalisia kwa manual ya manufacturer.

Manufacturer hatumii gari ikafika km laki mbili akajua inafananaje. Ataishia kuassimilate tuu.

Ni hali ya kawaida vikombe kutanuka na kupitisha oil. Gari nyingi ndogo zinakua recommended kutumia 0w30 kwasababu zinatestiwa nchini kwao kwenye baridi. Ukija kwa joto letu tunatumia kuanzia 5w30.

Baada ya kutumia kwa km nyingi utakuta oil inapungua kwasababu inapita mahali ambapo kwa umri (kilometers) wa engine panapitisha oil ila kiuhalisia hapakupitisha (haitakiwi kupitisha).

Baada ya hapo ndo ushauri wa kuweka oil nzito kidogo. Ila kama haipungui sana ni heri kuendelea na recommended.

NB: Sio ndo utoke 5w30 uende SAE 40, mjombaa baada ya muda flan utaishia kusonya tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…