Jinsi ya kuifanya gari yako itumie mafuta vizuri zaidi kuliko ulivyozoea

Jinsi ya kuifanya gari yako itumie mafuta vizuri zaidi kuliko ulivyozoea

Wakuu naomba kujua kuna madhara gani kutembelea gari ambayo ina ball joints zilizochoka (zinatoa mlio kama vigololi vinagongagonga) maana kwasasa mfuko hauko vizuri, na gharama zake za replacement zikoje kwa Spacio new model.
Ball joint nina uhakika mbili hazitazidi 40K, ukiwa na 50K unamaliza tatizo. Hio ndio raha ya Toyota mkuu hili chama ni burudani esp. ukiwa unamiliki gari jamii ya corrolla.
 
Hiyo namba 6(mfuniko wa tank la Petroli) unaweza shangaa tu sensors za ABS, CHECK ENGINE na CHECK VSC zinawaka ukabadili kila kitu haswa kama unatengeza kwa mafundi wapiga ramli na zisizime.. Ukicheck mfuniko unakuta uko loose ukizima na gari na kuufunga mfuniko vizuri kila kitu kinakaa sawa… ukinunua used inabidi kubahatisha sana ambao unaendana haswa na gari yako…
 
5. Weka engine oil iliyoshauriwa kutumika na wazalishaji wa hiyo gari
Kuna mtu engine yake inataka 5W 30 au 10W 30 ila kwa sababu anaona hizo engine oil zinauzwa gharama anaamua kuweka 20W 50 au SAE 40 yoyote. Jana nimemkuta mtu anaweka 20W 50 kwenye IST, aiseee ikabidi tu nicheke. Anyway unapoweka oil yenye grade kubwa kuliko iliyokuwa recommended unaifanya engine yako ifanye kazi ya ziada kusukuma hiyo oil na hivyo kuifanya itumie mafuta mengi zaidi.
Kuna mafundi/wauzaji wanatuambia tuweke 20W 50 kama kilometer zimezidi 150k hata kama manufacturer ame recommend 5w30, hili unalizungumziaje?
 
Kuna mafundi/wauzaji wanatuambia tuweke 20W 50 kama kilometer zimezidi 150k hata kama manufacturer ame recommend 5w30, hili unalizungumziaje?
Swali zuri
Nakutana na huo ushauri mara kwa mara.

Na mimi nasubiri jibu
 
Kuna mafundi/wauzaji wanatuambia tuweke 20W 50 kama kilometer zimezidi 150k hata kama manufacturer ame recommend 5w30, hili unalizungumziaje?
Hakuna fundi anayeelewa gari kuliko manufacturer.
Fuata maelekezo ya manufacturer
 
Habari Wakuu.

Leo nataka tuangalie mambo machache ambayo kila mwenye gari anaweza kuyafanya mwenyewe(DIY) ili kuhakikisha gari yake inatumia mafuta vizuri na hivyo kumpunguzia gharama.

Yafuatayo ni mambo ambayo kama ukiyafuata gari yako itatumia mafuta vizuri lakini pia italifanya gari lako kuishi maisha marefu.

1. Accelerate taratibu na pia funga brake taratibu
Usikanyage accelerator pedal kwa nguvu kama upo kwenye mashindano ya formula one na badala yake jenga speed ya gari lako taratibu na pia wakati wa kufunga brake funga taratibu. Kwa kifupi kadri unavyoipa shida(stress) engine yako ndio inavyotumia mafuta mengi.

2. Tumia mafuta ambayo mzalishaji wa gari alishauri yatumike
Kuna kitu watu wanaaminishana kwamba ukiweka premium inakaa sana kuliko mafuta mengine. Anyway, Kama waliotengeneza hilo gari walishauri uweke premium weka hiyo, kama walishauri uweke unleaded weka unleaded. Kitu kimoja ambacho unatakiwa kukijua ni kwamba haya magari huwa yanakuwa tested kila kitu kabla ya kuja kwa mtumiaji. Na kutoka kwenye hizo test ndio wanashauri kwamba tumia mafuta haya.

3. Usizidishe mizigo kwenye gari yako
Jitahidi kupunguza mizigo isiyo ya lazima kwenye gari yako kadri uwezavyo. Kadri unavyozidisha mizigo kwenye gari lako ndio engine inafanya kazi kubwa zaidi na kutumia mafuta mengi.

4. Hakikisha tairi zako zina upepo(Presha) sahihi
Kama tairi zako zitakuwa na upepo mdogo kuliko unaotakiwa basi tairi hizo zitakuwa zinazungushwa kwa shida kwa sababu ya kuwa na rolling resistance kubwa na hivyo kupelekea engine kufanya kazi kubwa kuliko kawaida na hivyo lazima mafuta yataisha haraka.

5. Weka engine oil iliyoshauriwa kutumika na wazalishaji wa hiyo gari
Kuna mtu engine yake inataka 5W 30 au 10W 30 ila kwa sababu anaona hizo engine oil zinauzwa gharama anaamua kuweka 20W 50 au SAE 40 yoyote. Jana nimemkuta mtu anaweka 20W 50 kwenye IST, aiseee ikabidi tu nicheke. Anyway unapoweka oil yenye grade kubwa kuliko iliyokuwa recommended unaifanya engine yako ifanye kazi ya ziada kusukuma hiyo oil na hivyo kuifanya itumie mafuta mengi zaidi.

6. Hakikisha mfuniko wa tank la mafuta unafunga vizuri na seal yake bado haijachoka
Kama mfuniko wa tank lako haufungi vizuri basi lazima mafuta yatakuwa yanaevaporate(kutoka kama mvuke). Hivyo mafuta yatakuwa yanaisha taratibu hata kama huendeshi gari lako. Hata kama mfuniko unafunga vizuri ila seal yake imechoka basi mafuta yataisha tu.

7. Endesha gari yako katika gear kubwa kadri uwezavyo
Endesha gari yako katika gear kubwa kadri uwezavyo huku ukihakikisha kwamba revolution ya engine yako inabaki chini. Kwa mfano gear namba 5 inaendeshwa na nguvu kidogo kutoka kwenye engine ukilinganisha na gear namba 1.

8. Jaza mafuta kwenye gari lako wakati wa asubuhi
Kama ilivyo kwa physical properties za za vitu vingine. Hata kwenye mafuta ni hivyo hivyo. Nayo husinyaa wakati yanapokuwa ya baridi na kutanuka wakati yanapokuwa na joto. Hivyo ukijaza mafuta wakati wa asubuhi unayo chance ya kupata mafuta mengi zaidi kuliko atakayejaza mchana au jioni.

9. Badili air filter katika muda sahihi
Kama air filter yako imejaa uchafu au imeziba, Engine italazimika kufanya kazi ya ziada ili kuruhusu hewa zaidi kuingia kwenye engine na hivyo itatumia mafuta mengi zaidi.

10. Kuwa makini katika kuchagua magurudumu(wheels) ya gari lako
Usichague wheels kwa sababu tu eti yana muonekano mzuri. wheels ni vizuri zikawa nyepesi, ngumu na kikubwa iwe na uwezo wa kusapoti uzito wa gari lako. Na katika hilo Alloy wheels ndio nzuri zaidi kuliko wheels zozote. Pia ni vizuri kuweka size sahihi za magurudumu kwa maana kadri unapoweka magurudumu makubwa zaidi maana yake unaongeza uzito kwenye gari yako na hivyo kuifanya engine itumie mafuta mengi zaidi.


MWISHO.iko juu sana hii
 
Hakuna fundi anayeelewa gari kuliko manufacturer.
Fuata maelekezo ya manufacturer
Usiukwepe uhalisia kwa manual ya manufacturer.

Manufacturer hatumii gari ikafika km laki mbili akajua inafananaje. Ataishia kuassimilate tuu.

Ni hali ya kawaida vikombe kutanuka na kupitisha oil. Gari nyingi ndogo zinakua recommended kutumia 0w30 kwasababu zinatestiwa nchini kwao kwenye baridi. Ukija kwa joto letu tunatumia kuanzia 5w30.

Baada ya kutumia kwa km nyingi utakuta oil inapungua kwasababu inapita mahali ambapo kwa umri (kilometers) wa engine panapitisha oil ila kiuhalisia hapakupitisha (haitakiwi kupitisha).

Baada ya hapo ndo ushauri wa kuweka oil nzito kidogo. Ila kama haipungui sana ni heri kuendelea na recommended.

NB: Sio ndo utoke 5w30 uende SAE 40, mjombaa baada ya muda flan utaishia kusonya tuu
 
Back
Top Bottom