Jinsi ya kuishi kwa amani na mwanamke aliyekuzidi kipato na kuifurahia ndoa

Jinsi ya kuishi kwa amani na mwanamke aliyekuzidi kipato na kuifurahia ndoa

Daaaah! Kitanda usicho kilalia hujui kunguni wake.

Hiyo kama ni elimu basi ni theory.
Fanya practical sasa uone machipukizi ya tabia za kila aina zitakazo ibuka, hawa viumbe hakuna formula maalumu ya kuishi nao.
 
Ili uishi na mwanamke kwa amani jishushe na uwe na kaunafki flani hivi lasivyo utazunguka kutafuta malaika wako
 
Kama kuna upendo wa agape kati ya wanandoa hao,pesa ni extra saana,..
 
Marahaba sana ila nimejikaza kusema haya. Wenye jinsia zao wakija watanipopoa mpaka nikome.
Kwa kweli ni tatizo kubwa sana kwenye jamii kwa sasa. Na tatizo linazidi kuongezeka kadri muda unavyoenda.
 
Zote mbwembwe tu, kuish na mwanamke wa aina hiyo nikua BWEGE TU
 
Habari za muda huu wapendwa,

Bila ya shaka sisi sote kwa namna moja au nyingine ni wahanga wa hili jambo kwenye jamii au ndoa zetu lakini ni wachache sana walio we za kuvuka salama salimini kwenye mtihani huu mambo yafuatayo yanaweza kukusaidia angalau kuishi na amani na mke kipindi ambacho huna kazi au amekuzidi kipato.

1) JIAMINI

Mwanaume asiyejiamini ni udhaifu mkubwa sana mbele ya mwanamke hii humfanya mwanamke asijihisi kuwa yupo salama mbele yako so kujiamini kwako kunamfanya awe na natumaini na wewe.

2) USIBADILI SANA RATIBA ZAKO

Kipindi ambacho huna kazi muda mwingi sana unakuwa idle hii hupelekea mwanamke kukuona kama wewe ni mtu ambaye umeshapoteza natumaini na umeshakata tamaa na maisha kwani huna jitihada tena za kuinuka tena hali hii humvunja moyo mwanamke na kumfanya ajihisi amebeba mzigo nzito sana hali ambayo huzaa msongo wa mawazo inayompelekea awe na hasira muda wote.

3) Mpe haki yake ya ndoa kwa utimilifu.

Umuhimu wa tendo hili unafahamika kwa wanandoa kwani huondoa stress na kufanya mwili kurelax hivyo basi hakikisha purukushani zako za kujikwamua kiuchumi wakati huu kwa kiasi kikubwa zisikuathiri utendaji wako wa chumbani.

4) Msaidie kuvaa asubuhi akitaka kwenda kazini.

Jambo hili humuondolea stress na kumfanya ajione yeye ni wa kipekee na ajione kuwa alifanya uchaguzi sahihi kuolewa na wewe (kumbuka wanawake wanafurahia mambo madogo ambayo kwa macho huwa yanaonekana hayana maana).

5) JIZUIE SANA KUTUMIA HELA YAKE KWA MAMBO YAKO BINAFSI

Nawasilisha
Aseee
 
Back
Top Bottom