Jinsi ya kujipatia kipato kupitia google adsense

Geoffrey Eng Atkinson

Senior Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
199
Reaction score
159
Habari zenu wana JF,

Ningependa leo kuzungumzia japo sio kila kitu ila mafanikio unayoweza kupata kwa kupitia google adsense, kwanza google adsense ni nn?

GOOGLE ADSENSE ni program maalum ilioundwa na google kwajili ya kuwawezesha wenye blogs, webistes, apps kujipatia kipato:
so kama nlivosema kwa wenye blogs, websites na apps, so pale utapokua unataka kujiunga unatakiwa uwe na moja wapo ya hivo,


NAWEZAJE JIUNGA NA ADSENSE?

-> Ili ujiunge na adsense unahitaji kua na blog au website au app, kwa leo tutaongelea upande wa blogs na websites, ukishakua na hio blog au website utatakiwa kutuma maomba kwenye page ya adsense ya kuomba kupata hii huduma na utajibiwa ndan ya mda flan, mara nyingi ni sku mbili au moja wengine mpaka wiki; utakapojibiwa tayar utapewa codes za kuweka kwenye blog au website yako, kuanzia apo utaanza kupata mapato yako

MAPATO YA ADSENSE YAKOJE?

-> Kwa kawaida hii ni biashara kama biashara zingine duniani , mapato yake hayapo kama ajira ila mapato yake yanatokana na juhudi zako katika blog yako, kwa mfano kwa siku unapata wageni 3000 kwenye blog/ website yako: apa wanatumia mahesabu yao wenyewe ambayo wamejiwekea uko google , lakini kwa haraka haraka yapo kama hivi ukipata wageni 1000 maana yake malipo yako ni kuanzia ($1 - $5) , na hii sio njia pekee tu ya mapato , njia nyingine unayoweza kupata mapato ni kwa clicks, ukishakua na matangazo kwenye website/blog yako hua kuna watu wanapenda kuona matangazo flan , kwa mfano anaeza ona tangazo labda gari linauzwa kwa bei anayotaka lazma ataclick apo aone nn kipo, au aanze kununua, sasa apa hua inategemea na mhusika wa tangazo ameweka budget ya bei gan, kuna clicks zenye bei ndogo sana kuna clicks zenye bei kubwa , kwa mfano kuna matangazo ambayo ukiclick unapata $1 per click mengine unapata $0.03 , so clicks utajumlisha na per 1000 views ulizonazo

KANUNI ZA ADSENSE KABLA HUJAJIUNGA?

-> mpka apo biashara inaonekana nzuri sana, ila kuna kanunia ambazo lazma uzifuate

1. Kuna watu hua wanaombaga mtu aiingie kwenye website yao ili waclick tangazo wapate pesa, ila lazma ujue kua google wanatumia vidakuzi(cookies) kwa hio taarifa zote zako wanazo na ni nyingi kuliko unavodhani, google wanajua kila mtu alieningia kwenye website yako alitokea kwenye computer gan na alitumia browser gan na ilikua mda gan na ulikua unafanya nn kwenye hio computer na vitu vingine vingi ambavyo huezi amini kama wanaeza jua, kwa mfano vidakuzi vya facebook hua vinajua watu waliopo pemben yako na namba zao za simu, ingawa hizi ni siri zao hua hawaziweki wazi ila vidakuzi ndio kazi zao, turudi kwenye mada, ukianza kuomba watu waingie kwenye website yako wakiclick account yako inafungwa na huezi irudisha tena na mapato yako yote yanafutika na ela zako wanapewa wenye matangazo!

2. Kukubaliwa kupata adsense sio kazi rahisi, sio kitu cha kutuma tu na kukubaliwa, kuna asilimia kubwa ya kukataliwa kama hujafuata sheria zao

3. kuna wengine wanadhan wakishakua na blog/ website basi wanaeza toa habari toka blog moja na kuweka kwenye blog yao, kwa taarifa yako, ukicopy post yoyote toka kwenye website yoyote duniani account yako inafungwa na mapato yako yote yanachukuliwa, kabla hujaomba hakikisha hujaiba chochote kutoka kwenye website yoyote duniani au blog

3. Makosa kama kuclick matangazo mwenyewe hayana msamaha zaidi ya mara mbili au moja, tunajua inaeza tokea ukaclick bahat mbaya labda ukiwa unaangalia muonekana wa blog au website ila ikitokea mara ya pili umefanya tena ivo account yako inafungwa na hutaweza irudisha tena


MAFANIKIO YA ADSENSE

-
> endapo utafuata kanuni za adsense vizuri we ni mtu ambae mafanikio ni yako, nilivokua kidato cha kwanza ndio nlijua adsense ila skuitumia vizuri kwa sababu ya utoto, nlikua na blog yangu ambayo nlitumia simu kuupdate, nlikua napata wageni zaidi ya 7000 kila sku, kwa siku mapato yalikua yanaenda kwenye $40 - $80 ila kwakua skua nafanya kwa moyo wote, mda mwingi nliutumia kusoma kwa ajili ya mitihan na nkaachana na hii bishara mpaka ilipokuja kununuliwa, mpaka sasa nliemuuzia anatengeneza ela nzuri kutoka kwenye blog, na hii inatokana na ule msemo wa "HATUJUI UZURI WA KITU MPAKA TUKIPOTEZE" nlivoona anatengeneza ela nzuri nkasema ntakuja kutengeneza blog ingine ila skupata mda , lakini nimeona niwape walau mwanga!

-> Yule alienunua blog alikua anatengeneza zaidi ya $4200 kila miezi minne hii ni kama 10 MILLION za kitanzania:

-> pia kuna baadhi ya website kama apa jamii forum wanatumia adsense kwenye matangazo yao, pia kuna wakina millard ayo: kwa mujibu wa website ya millard ayo inasema kua ana wageni 500,000 kila sku , na ni mmoja wa watu wenye adsense althoug anasehem nyingi ila kutokana na sheria za mapato ya adsense ina maana millard anatengeneza zaidi ya 1M - 2M kwa sku kwenye blog, pia kuna youtube channel yake , kuna mikataba ya makampuni:


Mpaka apo sina la ziada , nawatakia kila laheri kwa watakaochangamkia fursa kama hii
 
Ahsante sana . Nina swali kaka vipi kwa mfano umesoma kitu kwenye mtandao alaf ukaona kinafaa ukaamua kukiandika kwenye blog yako je hilo ni kosa?
 
Naomba kujua hv unaweza kutengeneza channel ya youtube na ukapata adsense bila ya kuwa na website/blog/apps na ikawa verified ukalipwa bila shida yyte
 
Mimi nashindwa kuelewa haya mambo nikifungua hata hapa jamiiforum nakutana na matangazo ya voda na mengine sasa sijui google ndio wanaruhusu hayo matangazo yawekwe kwako kutokana viewers au mfumo upoje
na lingine naomba msaada hivi naweza nikaomba google adsense kwa classified website
 
Naomba kujua hv unaweza kutengeneza channel ya youtube na ukapata adsense bila ya kuwa na website/blog/apps na ikawa verified ukalipwa bila shida yyte

yes: adsense ya youtube inasmama kama yenyewe na ya website inasmama kama yenyewe, na pia email utakaotumia kutengenezea adsense ya website unatakiwa utumie email tafaut ukifika kwenye youtube
 

Cha kwanza unapaswa ujue google adsense is a serious program na unapojiunga ni kama umeajiriwa ukiwa na CV SAFI: kuipata google adsense so rahisi na wala sio kazi ngumu cha msingi ufuate wanachotaka na unapata adsense: kuhusu jamii forum ipo ivi: unatuma request google kua una website inaitwa jamiiforum.com na unataka kua na adsense katika website yangu kwahio wao wanaiptia na baadae wakiona imekidhi vigezo vyote wanakupa code utakayoiongeza katika website yako: hio code hua ndo znadisplay ads wewe kazi yako itakua tu kudeal na webiste maswala ya ads ni kazi ya google, we kazi yako kuboresha website na kutafuta views, the more the view the more the $$, na kuhusu website ya classfied ofcourse yes inakubalika: ila wao wana vitu wanapitia katika hio webiste ndo wakupe go ahead siezi sema kama ukiwa na website ya classfied automatically utakubaliwa ila watakavoikagua ndo watakupa jibu and pia website kibao tu za classfied znatumia adsense cha msingi fuata kanuni na sheria zao
 
vizur but nimekula sana ela za adsense miaka km miwili iliyopita for now blogger sio ishu maybe youtube napo ni pagumu bila akili usione ni km easy ndugu yangu ila km una mda unaweza fanya na ukapiga mpunga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…