Zakaria Maseke
Member
- Apr 26, 2022
- 83
- 128
JINSI YA KUKAZIA AU KUTEKELEZA HUKUMU MAHAKAMA YA MWANZO:
Mwandishi: Zechariah Wakili Msomi
Zakariamaseke@gmail.com
(0612275246 /0754575246 - WhatsApp)
Unaposhinda kesi ya madai, mfano umefungua kesi na hukumu imetoka umeshinda kesi, labda Mahakama imesema ulipwe au urudishiwe nyumba, hauishii hapo tu, ili uweze kulipwa au kupata hiyo nyumba inabidi uombe execution (utekelezaji wa hukumu) wengine wanaita KUKAZIA HUKUMU. Ni kama unafungua kesi ya pili kumtaka mdaiwa aitekeleze ile hukumu.
Lakini inategemea, kama mdaiwa anakubali kulipa bila shuruti hakuna haja ya kurudi Mahakamani kufungua maombi ya kukazia hukumu. Utarudi Mahakamani kutafuta msaada wa amri ya Mahakama kama tu mdaiwa hataki kulipa kwa amani.
Sasa kuna tofauti ya jinsi ya kukazia hukumu za Mahakama ya Mwanzo na hukumu za Mahakama zingine kama Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama Kuu. Utofauti upo kwenye procedures (hatua), documents (nyaraka) na sheria (laws applicable).
Eneo hili kuna changamoto. Unaweza kuwa unaelewa vizuri jinsi ya kukazia hukumu ya Mahakama zote ila ya Mahakama ya Mwanzo ikakuchanganya. Na hii ni kwa sababu Mahakama ya mwanzo haifundishwi sana vyuoni wala law school. Lakini vivyo hivyo unaweza kuwa unaelewa vizuri jinsi ya kukazia hukumu za Mahakama ya Mwanzo ila za Mahakama za juu zikakuchanganya.
Kwenye makala hii utajifunza mambo yafuatayo:
1: Jinsi ya kukazia hukumu ya Mahakama ya Mwanzo
2: Sheria zinazotumika katika utekelezaji au kukazia hukumu za Mahakama ya Mwanzo.
3: Njia unazoweza kutumia kuitekeleza hukumu Mahakama ya mwanzo.
4: Nyaraka zinazotumika kutekeleza hukumu Mahakama ya Mwanzo.
1: JINSI YA KUKAZA HUKUMU MAHAKAMA YA MWANZO (HOW EXECUTION IS DONE IN PRIMARY COURTS)?
Hapa tunaangalia Procedure na documents (hatua na nyaraka).
Kama ilivyo kwa Mahakama zingine, hatua ya kwanza unatakiwa kuomba kutekeleza (kukazia) hukumu Mahakamani. Yule aliyeshinda kesi anatakiwa kupeleka maombi ya kukazia hukumu Mahakamani.
Unaombaje kukazia hukumu (how)? Kwa maana ya unatumia njia gani? Kwa mdomo au kwa maandishi? Kama ni maandishi hiyo nyaraka inaitwaje?
Kumekua na ubishani sana eneo hili, baadhi wanasema unatumia barua wengine wanasema unajaza fomu maalum ambayo utapewa pale Mahakamani au ambayo iko kwenye sheria inayotoa fomu maalumu zinazotumika katika mashauri ya Mahakama za Mwanzo inaitwa “the Magistrates’ Court (Approved Forms for the Primary Court) Rules, 2020”
(Kwa Mahakama zingine, maombi ya kukazia hukumu yanaweza kufanyika kwa njia ya mdomo au kwa njia ya maandishi (written form). Kwa mdomo kama madai yako yanahusu pesa (monetary decree) na huyo unayemdai mpo naye Mahakamani wakati amri ya Mahakama ya kumtaka alipe inatolewa. Ukisoma Order XXI rule 10(1), (1A). Na kwa maandishi kwa kujaza fomu maalum, FOMU NAMBA TANO (5) ambayo format au muundo wake unapatikana kwenye sheria inaitwa, Civil Procedure (Approved Forms) Notice, GN. No. 388 of 2017. (Hapa naongelea hizo Mahakama zingine).
Swali, je kwa upande wa Mahakama ya Mwanzo unatumia document (nyaraka) gani? Hilo swali nitalijibu kwenye kipengele cha mwisho.
2: SHERIA ZINAZOTUMIKA KUKAZA HUKUMU YA MAHAKAMA YA MWANZO:
Utaratibu wa kukazia hukumu za Mahakama ya Mwanzo unapatikana kwenye sheria zifuatazo:
(i) The Magistrates’ Courts Act (MCA) Chapter 11. (Sheria ya Mahakama za Mahakimu, sura ya 11). Hii ndiyo sheria mama ya Mahakama za Mwanzo. Kwa upande wa kesi za madai sheria hii imetaja mamlaka ya Mahakama ya Mwanzo kwenye jedwali la nne (fourth schedule) la sheria hiyo.
(ii) “The magistrates’ Courts (Civil Procedure in Primary Courts) Rules. Kwa kiswahili naweza kuziita Kanuni za Mwenendo wa Kesi za Madai Mahakama ya Mwanzo). Soma part III kuanzia Rule 56 - Rule 85.
Hii ni sheria ndogo (ni kanuni) zilizotungwa chini ya sheria ya Bunge (Act) inayoitwa Sheria ya Mahakama za Mahakimu (the Magistrates’ Courts Act kwa kifupi tunaiita ‘MCA’).
Kwa hiyo usitumie Civil Procedure Code (CPC) (Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai) Mahakama ya Mwanzo. CPC haitumiki Mahakama ya mwanzo isipokua katika mazingira maalum/machache saana (very rare and exceptional circumstances).
(iii) The Magistrates’ Court (Approved Forms for the Primary Court) Rules, 2020”. Hii ni sheria inayotoa fomu mbalimbali zinazotumika katika mashauri ya Mahakama za Mwanzo, zikiwemo fomu maalum kwa ajili ya kukazia hukumu.
3: NJIA ZA KUTUMIA KUKAZA HUKUMU MAHAKAMA YA MWANZO:
Unaweza kukaza hukumu ya Mahakama ya Mwanzo kwa njia zifuatazo;
(i) Kukamata na kuuza mali ya mdaiwa (attachment and sale). Soma Rule/Kanuni ya 56 ya Kanuni za mwenendo wa kesi za madai Mahakama ya Mwanzo na Aya ya 3(2) ya jedwali la nne la sheria ya Mahakama za Mahakimu (Paragraph 3(2) of the fourth schedule to the Magistrates’ Courts Act (MCA) Chapter 11).
Hakikisha mali unayotaka kukamata na kuuza inaruhusiwa kukamatwa kisheria. Kujua mali ipi haiwezi kukamatwa na kuuzwa soma Rule/Kanuni ya 63 ya Kanuni za mwenendo wa kesi za madai Mahakama ya Mwanzo na Paragraph 3(2) ya jedwali la nne la sheria ya Mahakama za Mahakimu (of the fourth schedule to the Magistrates’ Courts Act (MCA) Chapter 11).
(ii) Kurejesha na kukabidhi mali (Restitution and delivery of property). Soma Rule/Kanuni ya 58 ya Kanuni za mwenendo wa kesi za madai Mahakama ya Mwanzo
(iii) Eviction (kutolewa ndani ya eneo husika). Soma Rule/Kanuni ya 58 ya Kanuni za mwenendo wa kesi za madai Mahakama ya Mwanzo
(iv) Seizure of the property (kushikilia mali). Hakikisha mali unayotaka kushika inaruhusiwa na sheria. Soma Rule/Kanuni ya 56 ya Kanuni hizo hizo.
Ikitokea mdai anataka kushika au ameshika au amekamata mali ambayo hairuhusiwi kushikwa au sio yako wewe mdaiwa utafungua maombi ya kuweka pingamizi Mahakamani. Soma Rule/Kanuni ya 69 ya Kanuni za mwenendo wa kesi za madai Mahakama ya Mwanzo
Na ikitokea mdai anataka kushika au ameshika au amekamata mali ya mtu mwingine ambaye sio mdaiwa au asiyehusika na kesi utaratibu ni kama ule ule wa Mahakama zingine, unafungua kesi ya pingamizi (objection proceedings) kupinga mali yako kuingizwa kwenye kukaza hukumu. Soma Rule/Kanuni ya 70.
Ikitokea mali yako imeuzwa kwenye mnada kimakosa ili kutekeleza hukumu unaweza kuomba kutengua hayo mauzo. Kwa Mahakama ya Mwanzo utaratibu upo kwenye sheria yao hiyo hiyo niliyotaja mwanzo, “the magistrates’ Courts (Civil Procedure in Primary Courts) Rules.” (Kanuni za Mwenendo wa Kesi za Madai za Mahakama ya Mwanzo). Utaratibu na Mambo yote yanayohusu kukazia au kutekeleza hukumu za Mahakama ya Mwanzo yapo part III kuanzia Rule 56 - Rule 85 ya hiyo sheria.
(v) Njia nyingine ni kumkamata mdaiwa na kumfunga jela kama mfungwa wa madai (arrest and detention as Civil Prisoner). Soma Aya ya 4 ya jedwali la nne la sheria ya Mahakama za Mahakimu (Paragraph 4 of the fourth schedule to the Magistrates’ Courts Act (MCA) Chapter 11).
Kama ulifikri deni halimfungi mtu basi unajidanganya. Dawa ya deni ni kulipa tu hakuna namna nyingine.
Kama ilivyo kwa Mahakama zingine zote, vivyo hivyo ukishindwa kulipa deni kama ilivyoamriwa na Mahakama ya Mwanzo, mdai akitafuta mali zako akakosa, basi mdai anaweza kuomba mdaiwa ukamatwe na kufungwa gerezani kama mfungwa wa madai. Hii ndiyo njia inayotumika pale ambapo mdaiwa ni mtata ana uwezo wa kulipa deni ila hataki kulipa makusudi.
Wengine wanadhani njia hii inatumika mwishoni kabisa pale ambapo mdai amejaribu njia zote kudai kulipwa imeshindikana, lakini hilo linaweza isiwe kweli. Kwa sababu Majaji wanatofautiana sana katika kutafsiri sheria. Kuna baadhi ya Majaji wanasema huwezi kukimbilia kuanza kuomba kukaza hukumu kwa kumkamata mdaiwa kama mfungwa wa madai kabla hujajaribu njia zingine za kawaida. *Lakini Majaji wengine wanasema unaweza kuanza na aina yoyote ile unayotaka kukaza hukumu hata kama ni kumkamata mdaiwa. Ili kuondoa huko mkanganyiko kasome kesi za Mahakama ya Rufaa ambayo maamuzi yake yanawafunga mikono Majaji wote wa Mahakama Kuu na Mahakama zote za chini yake.
Hata hivyo, kuna utofauti kidogo ikiwa utaamua kukaza hukumu kwa njia ya kumkamata mdaiwa na kumfunga jela kama mfungwa wa madai. Ukisoma Aya ya 4 ya jedwali la nne la sheria ya Mahakama za Mahakimu (Paragraph 4 of the fourth schedule to the Magistrates’ Courts Act (MCA) Chapter 11) inasema (nanukuu);
“A primary court may, on the application of the party entitled to the benefit of such order in any civil proceedings, request a district court to take steps for the arrest and detention of any person who has failed to comply with an order for the payment of any amount, including compensation or costs, made by such primary court, and, upon receiving any such request, the district court shall have such jurisdiction and powers to order the arrest and detention of such order as if an application were made for the arrest and detention in the civil Prison of a judgment debtor in accordance with the provisions of the Civil Procedure Code.”
Kwamba, mdai anatakiwa kuiomba Mahakama ya Mwanzo kumkamata na kumfunga jela mdaiwa kama mfungwa wa madai, (hata hivyo mahakama ya Mwanzo haina mamlaka ya kutoa amri hiyo), badala yake Mahakama ya Mwanzo itatakiwa tena kuiomba MAHAKAMA YA WILAYA ichukue hatua za kumkamata na kumfunga jela huyo mdaiwa ambaye ameshindwa au amegoma kulipa deni la watu. Kesi itahamia Mahakama ya Wilaya na kuendelea kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai (Civil Procedure Code), kwamba sheria itakayotumika itabadilika na kuwa CPC?)
Hapa pia kuna ubishani, *baadhi wanasema huna haja ya kuiomba Mahakama ya Mwanzo kumkamata mdaiwa na kumfunga jela kama mfungwa wa madai kwa sababu Mahakama ya Mwanzo haina mamlaka ya kutoa amri hiyo, hivyo wanasema unatakiwa kupeleka maombi moja kwa moja kule Mahakama ya Wilaya ambayo ndo ina mamlaka. Na documents wanasema ni chamber summons na affidavit!
Wengine wanasema lazima upite kwanza Mahakama ya Mwanzo, alafu Mahakama ya Mwanzo yenyewe ndo itaona kuwa haina mamlaka na kuchukua faili na kulipeleka Mahakama ya Wilaya. Alafu wewe utaenda Mahakama ya Wilaya kila kitu utakikuta huko.
Wengine wanasema Mahakama ya Mwanzo ikishaona haina mamlaka, itatoa amri ya kukupa go ahead ya kwenda Mahakama ya Wilaya, alafu wewe utaenda kufungua maombi ya kutekeleza hukumu Mahakama ya Wilaya kwa kumkamata mdaiwa na kumfunga jela kama mfungwa wa madai, documents utatumia chamber summons na affidavit, utaambatanisha na ile amri na mwenendo wa Mahakama ya Mwanzo.
Na wengine wanasema Mahakama za Wilaya zimekua zikikataa mafaili kutoka Mahakama ya Mwanzo, zinayarudisha na kuwaambia Mahakama ya Mwanzo waendelee na kutekeleza hukumu hata kama njia inayotakiwa kutumika ni kumkamata mdaiwa na kumfunga jela kama mfungwa wa madai.
Sasa kipi ni kipi? Sina haja ya kueleza maana sheria iko wazi nimeshaeleza huko juu na nikanukuu kabisa. Soma tena paragraph 4 of the fourth schedule to the Magistrates’ Courts Act (MCA) Chapter 11).
Mwisho wa siku njia za kutekeleza hukumu ya Mahakama ya Mwanzo ni kama zile zile za Mahakama zingine. Tofauti ni sheria na procedures.
4: Kipengele cha mwisho ni NYARAKA ZINAZOTUMIKA KUOMBA KUKAZIA HUKUMU MAHAKAMA YA MWANZO:
Wengine wanasema barua na wengine fomu. Kipi ni kipi? Kwa kweli wote wako sahihi kabisa.
Mchakato wa kukazia au kutekeleza hukumu Mahakama ya Mwanzo unakua initiated (unaanza) na kundika barua ya kuomba kukazia hukumu. Alafu baada ya hapo maombi yatapelekwa kwa Mheshimiwa Hakimu ambaye anahusika kusikiliza maombi ya kutekeleza hukumu (anaitwa hakimu mfawidhi/in charge).
Baada ya hapo watakufungulia faili la shauri la kukazia hukumu, utapewa summons (wito wa kuitwa shaurini) utampelekea mdaiwa huo wito ili afike Mahakamani kujitetea kwa nini utekelezaji wa hukumu dhidi yake usifanyike, baada ya hapo kama hataki kulipa kwa amani, utaieleza Mahakama unaomba kutekeleza hukumu kwa njia gani? Utajaza fomu Maalum ya kuomba kukaza hukumu labda kwa kukamata mali za mdaiwa au kumfunga jela n.k. kutegemea na wewe umechagua njia gani. Utalipia gharama za Mahakama alafu mambo mengine yataendelea.
Kama utachagua kumkamata mdaiwa na kumfunga gerezani, bado utaanza kwa kuandika barua kuiomba Mahakama ya Mwanzo kutekeleza Hukumu. Ila utakapowaambia unataka utumie hiyo njia ya kumkamata mdaiwa na kumfunga mdaiwa au njia yoyote ambayo Mahakama ya Mwanzo haina mamlaka, wakishaona hawana mamlaka watakuambia uende Mahakama ya Wilaya.
Je, kuna haja ya kuambatanisha decree (tuzo) na hukumu (judgement) kwenye kukazia hukumu ya Mahakama ya Mwanzo? Kwa Mahakama zingine tunajua decree ni lazima, hakuna namna unaweza kutekeleza hukumu au hata kukata rufaa bila kuwa na decree (tuzo). Lakini kwa Mahakama ya Mwanzo hawana utaratibu huo kabisa, walau unaweza kuweka hukumu lakini decree haipo. Hata ukikata rufaa kama kesi imeanzia Mahakama ya Mwanzo hakuna ulazima wa kuambatanisha nakala ya hukumu au tuzo (decree) na haitakiwi kabisa, ingawa kuna saa Masjala/Makarani wanaweza kukazana na wewe wanakwambia lazima uambatanishe hukumu, kwa hiyo huwa tunaweka kukwepa usumbufu.
Kwa ufupi sana hizo ndo procedures na namna za kukazia hukumu kwa upande wa Mahakama ya Mwanzo.
Lipo andiko lingine kama hili refu zaidi ambalo nimeongelea jinsi ya kukazia na kutekeleza hukumu za Mahakama za juu kama vile Mahakama ya Wilaya, Hakimu Mkazi na Mahakama Kuu. Unaweza kulitafuta mtandaoni.
Asante kwa muda wako.
Imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zechariah Wakili Msomi (zakariamaseke@gmail.com)
(0754575246 WhatsApp).
-----MWISHO----
Ntoa angalizo, wale wazee wa kukopi machapisho ya watu na kuweka majina yenu. Ni kosa kisheria. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejimilikisha andiko hili. Unaruhusiwa tu kusambaza lakini usibadili yaliyomo. Ni heri uanze kuandika ya kwako mpya.
Disclaimer: Lengo la hii makala ni kutoa elimu kwa jamii. Huu sio ushauri wa kisheria kwa mtu yeyote. Kama unahitaji ushauri wa kisheria wasiliana na Mawakili. (Ikiwa kuna sehemu hujaelewa omba ufafanuzi au uliza swali, kuuliza ni bure kabisa).
Imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zechariah Wakili Msomi.
(0612275246 / 0754575246 - WhatsApp).
zakariamaseke@gmail.com.