Jinsi ya kulea vifaranga wa kuku wa kienyeji kwa lengo lako ni kuwa na kuku wengi?

Jinsi ya kulea vifaranga wa kuku wa kienyeji kwa lengo lako ni kuwa na kuku wengi?

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Leo natamani kutoa elimu juu ya malezi ya vifaranga wa kuku wa kienyeji ili kupata tija. Napenda niwatoe wasiwasi kwa kuwajulisha kuwa haya mafundisho nitakayoyatoa nimeyasomea ( Agricultural science) na pia nimeyafanyia uchunguzi.Natamani yale mafupi sana ila yenye ubora

Kwanza kabisa napenda kutoa elimu ya kutumia mtaji mdogo na matumizi ya mazingira yanayomzunguka mtu ili aone faida yake na akupe mtaji wake kulingana na uwezo na mahitaji yake.

Hatua za kuzingatia ili kulea vifaranga wako vyema ni kama ifuatavyo:
1. Baada ya vifaranga kuangaliwa unapaswa kuandaa mazingira mapya mfano box.

2. Andaa chanzo cha joto mfano chungu weka jivu kisha fukia mkaa unaowaka weka pembeni ya box.

3. Weka tandiko ndani ya box kisha weka pumba laini ndani ya box.

4. Vinyweshe vifaranga glucose au maji yenye glucose asubuhi.

5. Viingize vifaranga kwenye box.

6. Baada ya siku mbili anza kuvipa pumba laini bila maji na badala yake viwekee maziwa fresh na kisha vipe tena maji.

Endelea kufanya hivyo kwa mwezi mmoja kisha nipe mrejesho.Lengo hapa ni kuhakikisha Tembe anaangua vifaranga na kutipoteza muda kulea vifaranga ili atage tena na kuangua tena.Ila hakikisha tembe wako na jogoo wanakula vizuri vyakula vyenye protini, maji, wanga, mafuta ,maji na matunda.

Tanbihi: Kuku huhitaji virutubisho vyote sawa na anavyohitaji binadamu pamoja na usafi.
 
Unavinywesha vipi? unakishika na kukifungua mdomo? au unaweka kwenye sahani/chombo chochote accordingly wanakunywa wenyewe?
Vinakunywa vyenyewe ila mwanzoni ukiona inasumbua jaribu kuvinywesha kwa kupanua mdomo ila usivipe mengi sana.
Vyakula vya majimaji mengi siyo vizuri sana kwa kuku.
 
Maziwa fresh tena? Sijawahi sikia
Naam na ni vizuri uyachemshe ili kulinda kuku wako wasisumbuliwe na typhoid mara kwa mara.Jaribu utakuja kuweka majibu yako hapa.
Nimefanya majaribio kadhaa nimeona matokeo ya uhakika na ninakuhakikishia kuwa ukiwapa kwa usahihi utafanikiwa sana.
 
Maziwa yanasaidia nini na unawapa kwa muda gani?
 
Maziwa yanasaidia nini na unawapa kwa muda gani?
Mwezi mmoja inatosha ila wakizoea hata wakiwa wakubwa unawapa mara chachechache.
Baadhi ya sifa za mazoea ni:-
Maziwa yana madini
Maziwa yana amino acids,calcium na protini.
Maziwa yana virutubisho vingi mno zaidi ya hivyo ambavyo ni muhimu kwa kiumbe hususani kipindi cha uchanga.
Tanbihi : Tafiti zinaonesha kuku wana uwezo Mdogo wa kumeng'enya lactose.
Badala ya kuhangaika kutafuta damu chokaa dagaa n.k njia mbadala na rahisi ni kuwapatia maziwa na pumba laini.
Jaribu nina uhakika na ninachokitolea ufafanuzi.
 
Maziwa lwa ajili ya nini? Acha upotoshaji Dogo ndo shida ya copy and pest.

Eti wape pumba bila maji, hahaaa acha upotoshaji, inaonekana hujawahi fuga wewe
 
Maziwa lwa ajili ya nini? Acha upotoshaji Dogo ndo shida ya copy and pest.

Eti wape pumba bila maji, hahaaa acha upotoshaji, inaonekana hujawahi fuga wewe
Ninachokifanya nakielewa Dogo sijawahi kubahatisha kama umekaririshwa mambo utakuwa umekosea sana.

Kitu kama hukielewi tulia uone waliofanya wanafanyaje na kama una jambo la kuongezea unaweza kuchangia siyo kuleta kebehi za kipumbavu.

Kama ukitaka ushahidi njoo nikuoneshe na matokeo yake.Sijajifunzia haya kwenye maduka ya kilimo na mifugo ( ninaelewa ninachofanya).

Weka sehemu uliyoona nimecopy na ku- paste hapa usipende mambo ya kutafuta sifa za kituo humu.
 
Hapa umempa za uso fresh manaake wabongo kila kitu kupinga utazani wanaweza kitu

Back
Top Bottom