Jinsi ya kumfahamu girl anayekupenda.

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
JINSI YA KUMFAHAMU GIRL ANAYEKUPENDA.
Siyo kwamba ishara hizi zote anaweza kuwanazo msichana mmoja,ila kila mmoja kwa ishara zake

Hatua hizi zinaweza zikakusaidia kumgundua msichana anayekupenda,wasichana wanatofautiana ila wengi wao wana-share ishara tofauti.
1.Mnapoongea:
Sikiliza sauti yake,kama anaona aibu sauti yake itakuwa ya upole/laini.
anaweza akaanza kushika shika nywele zake au kuweka sawa mavazi yake.
Hawezi akakuangalia machoni atakuwa anakuangalia kwa kuibia.
Msichana anayekupenda anakuwa na tabasamu unapoongea naye kama amekuzoea,
ila kama hajakuzoea anapokuona gafla tabasamu hutoweka maana anakuwa na aibu.



2.Anapenda hugs na kukushika:

Unapotembea naye mahali anapenda kushika mkono wako,au unapokutana naye
anaweza kuhug.

3.Ajali za kijitakia
anaweza akaona kitu kidogo tu au mdudu halafu anakurukia,au anakukumbatia.
anaweza akatafuta sababu yoyote ilimradi tu akushike,atajitahidi usigundue
mbinu zake kwa kupotezea "Ooh i'm sorry i didn't mean it"


4.Anaibia kukuchunguza:
Unapokuwa umetulia zako unakuta anakuangalia kwa kuibia,ukigeuka anajifanya yuko busy na mambo
yake kumbe anakuchunguza taratibu


5.Wangalie marafiki zake.
Anapokuwa na marafiki zake akikuona anaweza akajitenga,hata kama mmeenda out pamoja na marafiki
zake utakuta yupo karibu na wewe,akiwa na marafiki zake halafu mkakutana gafla atakufuata halafu
waangalie marafiki zake utakuta kama wanateta,ukiona hali hiyo kuna siri yao yeye na marafiki zake
kuhusu wewe


6.Anapenda umjali.
Anapokuwa na tatizo au anajisikia vibaya lazima akuambie,mfano mmeenda mahali kukawa na baridi
hata kama si baridi sana atasema anahisi baridi ili mradi umsaidie koti lako,hata kama kuna watu
hawezi kuona aibu kuvaa badala yake atajisikia vizuri anapovaa koti lako.

7.Hawezi kuzuia tabasamu.
Unapomwonyeshea tabasamu lazima na yeye akuonyeshee,hata kama kuna kitu kimemwudhi
atakuonyeshea tabasamu ili mradi aonyeshe umemkuta katika hali ya furaha.


8.Ishara za mwili.
Anapopita mbele yako anaweza akafanya madoido mengi ambayo yatakuvutia ila kama anajiamini.
kama hajiamini anapokuona gafla anakosa amani,utamwona anashtuka gafla.


9.Anafurahishwa na vituko vyako.
Huwezi ukamboa,hata kama ukifanya kituko ambayo haichekeshi utakuta anafurahia.





10.Anakujali:
Anakuwa anakujali,mfano akiona umeumia labda umejigonga,yupo radhi akuhudumie.
unapokuwa naye anaweza kuuliza..."unahitaji chochote?....unaweza ukasema "nina kiu ngoja ninunue maji"
utamsikia "nina maji,kunywa haya yangu kwanza".basi ujue kwamba anakujali.





NB:Kama hujampenda unaweza ukajiepusha naye hatua za mwanzo ili msiende mbali na kuingia kwenye mahusiano ya kumwumiza hapo baadaye,Wengine wanaweza kufanyiwa hizo ishara zote na wasiweze kugundua,Cha msingi unatakiwa uwe na mda wa kumsoma mpaka pale atakapokuzoea kabisa na akaanza kushindwa kuficha hisia zake,siyo rahisi kwa wanawake wengi kumwambia mwanaume direct kuwa anampenda,baada ya kuona dalili zote unaweza kumtongoza na kumtamkia unampenda utakuwa umemrahisishia kazi.











 
Hivi kuna galz na ladies eeh? Manake wengine maswali mwanzo mwisho hakuna aibu,lol!
 
Anayenipenda? Ina maana bila hizo dalili sijapendwa bado mkuu?
Haya mambo yapo very complicated,it z not easy to say for sure
kuwa huyu amenipenda coz kuna wengine ktk malezi/makuzi yao hizo
ni dalili za kawaida sana kwao kuwaonyesha wanaume na wanakuwa
hawako in love at all.
Kama vile watu ambavyo huwa tunachanganya kati ya UPOLE na UKIMYA,
ndivyo inapokuwa vigumu kuzielezea dalili za mtu anayependa generally as
you have just done.
Ili ujue kuwa unapendwa,lazima kutakuwa na some "chemistry" btn you two
ambayo ni vigumu kuielezea BUT its easy kui feel.
 
Mie hata hayo mambo ya u-gelo nakumbuka basi my dear? Ya kuchuma vijani sijui na nini? Niliruka stage, ukinirudisha kwenye sup saa hizi utaniumbua banaa! Mie nikikupenda naanza kukuambia kuna shamba linauzwa, tafuta ng'ombe wa mtamba na sungura wa maziwa.
King'asti hebu saidia hapo kwenye hizo dalili,mawazo yako pliiiz!
 
aaahhhh wanawake bwana shida zote hizi za nini?

Ukimpenda mwanaume unamwambia na ukimtamani pia unamwambia tu.....

Sio kila mtu ana uwezo wa kusoma ishara
 
aaahhhh wanawake bwana shida zote hizi za nini?

Ukimpenda mwanaume unamwambia na ukimtamani pia unamwambia tu.....

Sio kila mtu ana uwezo wa kusoma ishara

Tatizo ni kwamba mwanamke huyo akishafunguka nyinyi wenyewe mnamtoa confidence kwa kumdharau,au kwa kumjibu makavu...wengine ndo hadi wanaenda kuwaambia washkaj zao,kisha wanamcheka na kum discuss kila wakimuona..ndo wengi inakuwa ngumu.
 

Chukua 96%
 
King'asti umeniacha hoi!!!
 
Last edited by a moderator:
Pochi lako likiwa hivi hakuna mwanamke duniani ambae hatokupenda:


“A successful man is one who makes more money than his wife can spend. A successful woman is one who can find such a man.” - Lana Turner

Kama unabisha muulize MadameX.


 
Last edited by a moderator:
Pochi lako likiwa hivi hakuna mwanamke duniani ambae hatokupenda:

"A successful man is one who makes more money than his wife can spend. A successful woman is one who can find such a man." - Lana Turner

Kama unabisha muulize MadameX.



Absolutely true, no further discussion on this!
 

i strongly agree with u
 
Last edited by a moderator:
HUYO NI KUTOKA IRINGA! WALE WA IFM NI TOFAUTI ANAKUCHANA LIVE! i.e NIMEKUZIMIA MTU WANGU, MTU KAMA WEMA SEPETU AKIKUPENDA ATAANGALIA CHINI HUYO?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…