Unapokuwa kiongozi, hasa wa siasa, unapaswa kuwa makini sana hasa na viongozi ambao watajifanya ni rafiki zako kumbe wanatafuta tu namna ya kukuchonganisha na wananchi. Na hili namwambia wazi Raisi Samia ajihahdari sana. Sifikiri kwamba viongozi wote, na hasa wateule wake, wapo pamoja naye siku zote kama ambavyo wanamfanya aamini.
Wapo viongozi ambao watamwambia Raisi Samia sisi tuko nyuma yako twende tu mama - lakini anapaswa kuwaambia wazi huko nyuma yangu mnafanya nini, njooni tuwe bega kwa bega ili nione mnachofanya.
Kuna mambo ya msingi manne ambayo Raisi Samia anapaswa kuwa nayo makini sana. Haya ni mambo ambayo yatamfanya aungwe mkono au kuchukiwa na wananchi kwa ujumla. Haya mambo ni;
- Suala la tozo/kodi za serikali
- Suala la Katiba mpya
- Suala la uonevu wa Polisi (pamoja na haki za binadamu)
- Mambo ya Muungano
Katika haya manne, nakuambia wazi Raisi Ramia, tread with care, la sivyo yanaweza kukuharibia sana rekodi yako ya uongozi wa Tanzania. Usiwe mwepesi kupokea ushauri wa wateule wako juu ya mambo haya manne, wasikilize, na kama ikibidi kupata ushauri ni vema upate ushauri nje ya watu wanaokuzunguka, wasio na maslahi ya moja kwa moja katika uamuzi wako juu ya hayo mambo. Na pia, lolote utakaloamua weka Tanzania na Watanzania first without separating the two. A seemingly good thing for Tanzania might not be a good thing for Tanzanians, and vice versa.
Acha matamko ya harakaharaka juu ya mambo haya, tafakari kwa makini kabla hujaongea lolote kuyahusu. Na sio lazima uende na masimamo wa chama chako katika haya mambo manne. Wapo wanaokuzunguka watakaotaka kukukaanga kwa mafuta yako mwenyewe kupitia haya mambo manne kwa kutumia moto wa chama chako - be warned.