Jinsi ya kumkosanisha Rais Samia na Watanzania na kumfanya achukiwe: Tozo za Serikali, Katiba Mpya, Uonevu wa Polisi, Mambo ya Muungano

Hivi kwa nini tunapoongelea katiba na uonevu wa polisi wewe unaona ni mambo yanayohusu wapinzani peke yake? Kwanza kwa hilo tu unaonyesha wazi huna upeo wa kuona mbali
 
Twende Polepole....

Samia hawezi kuwa mtaalamu wa kila kitu..., Samia ana wasaidizi wake ambao wanatakiwa kumsaidia wakiwemo wabunge..., Hivyo kama Bunge limepitisha imefika kwake ni rahisi na yeye kuipitisha.

Hilo halimkatazi wala halimzuii kubadilisha mawazo kwa kuona kwamba ushauri alioshauriwa na watu wake haukua sahihi..., After all wa kuwasikiliza zaidi ni wananchi amabao theoretically ndio wabunge wanaowawakilisha...

Hivyo basi kubadilisha kwake maamuzi ataonesha ukomavu zaidi kuliko kungangania maamuzi mabovu sababu tu eti yalishafanyika...
 

Umesahau swala la loan board kiongozi,Mh Raisi aliwaelekeza loan board wafute value retention fee lakin mpaka dakika hii wameshindwa kutekeleza jambo hilo,sasa hawa loan board wanamchonganisha Mh Raisi na wanufaika
 
Umesahau swala la loan board kiongozi,Mh Raisi aliwaelekeza loan board wafute value retention fee lakin mpaka dakika hii wameshindwa kutekeleza jambo hilo,sasa hawa loan board wanamchonganisha Mh Raisi na wanufaika
Kumchonganisha na wasomi wa nchi hii!
 
UPUUZI MTUPU!!! Havijui vipato vya Watanzania? Mbona Watanzania wengi tu hatuna wasaidizi tulipoona tu hizo kodi tukajua ni UPORAJI wa mchana kweupe? Huhitaji wasaidizi kujua hiyo kodi ni WIZI.

 
Maria Sarungi ujuaji umemjaa. Rais kukubaliana na matakwa ya watu ndio uongozi wenyewe kwani haongozi kuku wala panya anaongoza watu wenye maoni yenye kubadilika kutokana na mahitaji yao.

JPM alichukiwa kwa misimamo yake isiyoyumba mpaka akaitwa dikteta uchwara leo Samia anakuwa msikivu bado mtanzania analalamika, labda waje malaika waiongoze nchi yetu.
 
Acha uongo
Yeye mwenyewe kuna siku alisema Kodi ya sh 100 iliyoongezwa ni ndogo sana, hivyo watu walipe tu.
 
Acha uongo
Yeye mwenyewe kuna siku alisema Kodi ya sh 100 iliyoongezwa ni ndogo sana, hivyo watu walipe tu.
Kodi imeongezwa mia ? na Wapi ?

Tunaongelea Kodi ya Miamala hapa imeongezwa kiasi kwamba watu kuacha kutumia huduma ya miamala sababu option nyingine ni cheaper zaidi)
 
Hivi kwa nini tunapoongelea katiba na uonevu wa polisi wewe unaona ni mambo yanayohusu wapinzani peke yake? Kwanza kwa hilo tu unaonyesha wazi huna upeo wa kuona mbali
Niandikie vifungu vitano tu vya katiba ya sasa na athari zake ambazo ww unaona havifai, ili na mimi niweze kuona hicho kisichofaa kweny katiba ya sasa, maana mmeshazoea kulishwa maneno bila kujua faida na hasara ya kile mnacholishwa. Kuhusu uonevu wa polisi pia kuna sheria za kufuata kabla ya mtu au watu kuandamana au kufanya mkutano wowote wa hadhara. Watu wanapofanya mikutano au kuandamana bila kibali ni lazima wakutane na mkono wa sheria waadhibiwe ili iwe funzo kwa wengine. Hii nchi ina sheria zake na lazima zifatwe na kuheshimiwa.
 
Kama unafikiri kwamba watu wanataka Katiba mpya kwa sababu ya sasa haifai basi wewe ni kihiyo hupaswi hata kufungua mdomo wako watu wanapoongelea Katiba.

Watu wanataka Katiba iliyoboreshwa, ikiwezekana kupunguza, kuongeza au kuboresha.

Kumbe kuna watu hamjui kitu ila mnashabikia tu ooh, hatutaki Katiba mpya. Anaelishwa maneno nani sasa kati yetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…