Jinsi ya kumtambua ng'ombe wako kama yupo joto

Jinsi ya kumtambua ng'ombe wako kama yupo joto

mchau

Member
Joined
Nov 16, 2024
Posts
89
Reaction score
95
Habari wafugaji, Leo tutajifunza juu ya kumjua ng'ombe wako Kama yupo kwenye joto (estrus),

dalili za joto kwa ng’ombe:

1. Kukubali kupandwa (standing heat):
- Dalili kuu! Ng’ombe husimama kimya anapopandwa na wenzake au dume.

2. Kutoka ute mwepesi (clear mucus) sehemu za siri
- Mara nyingi ute huu hushuka hadi miguuni.

3. Vulva kuvimba na kuwa nyekundu

4. Kupungua kwa kula na kushuka kwa uzalishaji wa maziwa

5. Kuchanganyikiwa/kutotulia, kurukaruka, na kupiga kelele

6. Kunyonyesha wenzake au yeye kunyonyeshwa

7. Kukojoa mara kwa mara

8. Kushusha mkia mara kwa mara na kupinda mgongo

Karibu sana kwenye huduma zetu bora za mifugo.
Kwa mawasiliano zaidi
0674740836
0792263640
 
How about silent heat?
Swali zuri sana kama mnyama wako anakuwa anaingia kimya kimya kwenye joto njia Bora ambayo tunatumia tunamchoma hormones ambayo inamfanya aingie joto Tena ili kuweza kufanya zoezi la upandishaji .
Hii changamoto inawakuta wafugaji wengi sana wanashindwa kufanya zoezi la upandishaji kwa sababu hawajui Kama mifugo wake yupo kwenye joto.
👉Njia Bora tunamchoma hormones ya kumuingiza joto iwapo mifugo wako inaingia joto kimya kimya bila kujua
 
No 2, 5, 7 na 8 ni uhakika kabisa, Mie ni mfugaji.
Ndiyo mifugo wako anaweza kuonyesha dalili kadhaa za kwamba yupo kwenye joto.kwa hiyo unahitajika kuwa makini pindi unapomuangalia mifugo wako
 
Back
Top Bottom