Am sure unaongelea vijijini ambako bado wanaishi miaka 500 BC. Kha! Hapa town mwanamke gani utamuaga unaenda kutongoza???
nyumba kubwa, huwezi jua kama hakuna mtoto wa nje.
Ila inawezekana aliwapiga marfuku kukanyaga hapo kwenu, kuna watu wanafamiana misibani.
Kuna dada mmoja mkubwa, alikutana na mama mmoja mtoto wa baba yao. Yule dada wa nje akajitambulisha. Yule dada akamjibu, tusijuane.
Mie nikamshangaa, unakataa faida? Mtu mzima, anataka tu mfahamiane sababu mnashare baba unamfukuza? Wala hakutegemei??
Mtu akitoka hapo kwa Mwingira, anaomba upendo wa baba, anyway nisiseme sana but wizi mtupu.
ni asilimia ngapi ya Tz ni mjini ukilinganisha na vijijini?
May be? Kama yupo na hatumjuhi ni sawa na ha exist tu.
Ila si tulikuwa wapekuzi kweli (not our mum) hivyo tulikuwa tunavijua vishtobe vyake karibu vyote ...sijuhi wengine bankers, ma air hostes (ATC those days) na hakuna alokuwa na mtoto.
Kuna wanaume wako makini.Lol. Wanachiti responsibly...mfano baba yetu mpaka natoka home hajawahi kulala nje...na anajisifu kwa hilo...anakwambia mwanaume ulo kamili huwezi kulala nje ya nyumba yako au kula kwa watu.
Hivyo hao vicheche wake uhusiano ulikuwa unaishia bar na guest tu.
hakuna forumula
Kongosho tunayoongelea humu tunaongelea kuhusu wanawake na wanaume wa kisasa...tukisema tu generalize kila tunachochangia mpaka vijijini kila kitu haki apply. Hivyo tunaongelea kuhusu mimi wewe na yeyote mwenye access na utandawazi kwa kiwango kikubwa kwa maana anayejua kuwa tuko 21 century
Kongosho waambie ile niliyotumia kwako, maybe inaweza kuwa ndio formula yenyewe.
Hakuna kheri juu ya shari. Mimi nilimleta nyumbani na kumwambia huyu mtoto wangu. Akanuna wiki nzima mimi sikujali, kisha akasema mume wangu umenikosea sana. Nikajibu kwa kifupi pole kisha nikauchuna. Hadi leo mtoto yupo. A cub cannot lead the Lion.
Mwisho wa siku kila mtu ana maamuzi na maisha yake...nyumba yangu si ya intruders...sikulelewa katika hayo mazingira hivyo kama nitasamehe msamaha wangu hauta include kulea mtoto wa nje...atalelewa na mama yake for his/her own sake nadhani nimeeleweka...siwezi mpenda mtoto wa nje kama mwanagu hiyo ni black and white to me.
Kuna majambo yanayowasibu wanaume wengi katika pitapita zao na kung'angania nyumba ndogo wanajikuta wanapata watoto nje ya ndoa ni njia ipi ya kistaarabu ya kumtambulisha mtoto wako wa nje kwa mkeo unayempenda????????
Njia ya kistaharabu? Kuna ustaharabu tena hapo wakati ushaharibu? Njia yeyote utakayotumia lazima kinuke tu; whether utapika pilau na sherehe ya kumuingiza mtoto ndani; whether utamleta kimya kimya...kosa liko pale pale.
La kwanza ni usiri...maana unauliza kumleta ndani meaning umeshindwa hata kumfahamisha mkeo uwepo wa huyo mtoto unataka kuja na suprise kubwa kuliko. Lol. Mi naona ni very rude...kuzaa nje umeamua mwenyewe ...na whether mtoto anakuja ku wa join wenzie or not unataka tena kuamua mwenyewe.
Ukipata mke kichaa atapishana na mtoto mlangoni...anaingia yeye anatoka.
dunia hii full unafiki.
Wanamme wako disadvantaged kuhusu watoto wa nje. Wao wakizaa inajulikana from day one.
Ni wanamme wangapi wanalea mamluki??
Ukifikiria hapo tu, hutaona haja ya kumnyima mwanamme kukaa na mwanae.
ha ha ha, afu wewe
uje umchukue kabisa, kwanza hata matumizi hutoi.
anitambulishe ili kiwe nini?nimlee?hapana jamani sina hicho kifua cha kule mtoto wa mwanamke aliyeingilia ndoa yangu!baki huko kwa moyo mweupe!