kwanza Elimu siyo kigezo cha kutafuta mchumba unless ukiwa materialist nasema hivi kwa sababu
1. wapo wenye elimu za vyou vikuu lakini (hawana elimu ya maisha) hawawezi kutunza familia zao ( hadi malecturer wa vyuo wamo tena wenye PHD). Kazi yao kulewa pombe, kuchuka vyangu doa, wanawapiga wake zao, hawana muda wa kukaa na familia zao na hata wengine kulipa ada ya mtoto wake ni tatizo. Hujaona watoto wa watu wenye madigirii wanakua wapiga debe? Sasa`kama mwanamke unafuata kigezo cha mume ni elimu basi uwe makini ( mmmh! kwa hiyo hata kama hujampenda kisa dr. unamkubali?) du!!! hii kali
2. wapo wasio na elimu ya darasani ila wana elimu ya maisha (wanaongea kwa mantiki na busara na wanafanya mambo yao kimikakati)
3. Na wapo wasio na elimu ya darasani na ya maisha, sasa hawa ndiyo kila mwanamke anatakiwa kuwa nao chonjo wakati wa uchumba, kawa bwana mara nyingi hawaelewi maisha na vigumu kubadilika kabisaaa!
Cha msingi nadhani ni upendo uanze halafu hayo mengine yanafuata.
Ni kweli kuishi na mwanamke aliyekuzidi elimu ni ngumu sana kwa sababu ya hulka zao. Mara nyingi mwanamke hupenda kumsifia mume wake kwa wenzake, sasa kama kidato hakijapanda ndugu yangu na huna mavumba ya kutosha, hapo huna ujanja. Utapigwa chini coz hurembeki kwa mwanawake wenzake. Nafikri pia wanawake wanathamini sana wenzao wanawaonaje kuliko wao wanavyojiona na hapo ndiyo tatizo linaanza. Wengi wao wanataka kuwa matawi ya juu kila wakati bwana!