Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Nawezana..Mkuu..Basi TU nikiona wadada kwa mitandao wanaflat tummy najiona Kama nakosoro flani hivi...Pia kiafya Sio nzuri..
Pole sana aisee tumia green tea naskiaga wadada wanasema inasaidia au tafta Clean 9 ya forever living uwe kama Wema Sepetu wa sasa.
 
Achana na maneno ya waswahili.mirungi ni miti ya peponi inaliwa ulaya na ulimwengune kote.
kulakitu shamba apunguze mwili.handas ikipanda dunia yote utaona niyako nawewe ndo malkia wa enzi na enzi.
Hahahahah Full andhas!😂😂😂
 
Situmii pombe kabisa mkuu... Nanyama hua nakula Mara mojamoja Sana... Kwetu Ni ma vegetarian..
Kitambi ni matokeo ya kula sana, yaani kula zaidi ya mahitaji ya mwili, over feed au kwa lugha nyepes Ulafi, au uroho, punguza kula, hayo mazoezi yanaweza yasikusaidie, nimeshaona mtu anafanya mazoezi halafu anakula sana, kitambi kitaenda wapi ?, pia nasikia kufany mazoez huwa kunaongza hamu ya kula, pungza kula halafu fanya kai nguvu kwenye jua kali kuanzia asubuhi mpaka jioni shinda kwenye jua na uhakikishe unatoka jasho mwil mzima kila siku utarudi hapa kunishukuru
 
acha kula wali na ugali hayo mawanga ndo yanajaza tumbo lako dear
Kwahio aendelee kula chapati na mandazi vyakula ambavyo vimebeba mafuta kwa wingi and still vyenyewe ni wanga. Yani bora hata ugali kuliko hayo makarangizo
 
Lala chali mwambie mtu akushike miguu yako kwenye mapaja ili yasinyanyuke,uwe unaamka mwenyewe kuja juu,fanya hivyo mara 15 asubuhi na jioni,baada ya wiki moja njoo utoe mrejesho...
 
Halafu kula si tatizo sana, ishu ni shughuli gani huwa unafany baada ya kula. Au unatazama Sultani tu ukiwa juu ya kochi hadi unasinzia.
Aisee... shughuli za kunitoa jasho Ni chache Sana.... Hivyo nakua sedentary muda mwingi
 
Nimekusoma vizuri, na wala sijakukashifu, labda kama uniambie kukupa taarifa uwa hujui unachokula umechukulia kama kashfa

Kazi ya protein siyo kunenepesha mwili ni kajenga mwili, ku repair tissues, organs na mifupa, protein supplements mnazopewa ni kwa ajili hiyo ndio maana unaona misuli inakaa sehemu yake.

Ukizidisha protein pia utazidisha kitambi kwa maana chakula kikishaingia mwilini kinabadilishwa kuwa energy, ukishindwa kuitumia itabadilishwa kuwa mafuta na kuhifadhiwa na mwili kwa matumizi ya baadae. Ukisave hizo energy unakuwa na utajiri wa mafuta.

Cheki mabaunsa wanaoshinda gym ila bado wana vitambi.
Tissue haiwi repaired na protein tupu. Ingekua hivyo steroids na HGH zingekua na protini tupu.

Narudia tena. Kabohaidreti (Ubwabwa, ugali, viazi n.k) ndiyo nguvu yako. Protini ndiyo inasababisha kuongezeka (kunenepa kwa mwili)

Notisi kwamba nimesema kua kula chakula kingi hakuna madhara kama unafanya mazoezi ya kuendana na chakula unachokula. Hao mabaunsa wenye vitambi hata siyo kwaajili ya kula mostly ni kwaajili ya supplements na yes am saying it hata supplements kama haufanyi mazoezi ipasavyo mwisho ni kutokwa na kitambi.

Niliandika uzi juu ya supplements katika bodybuilding. Nimeutafuta siuoni ila najua juu ya nutrition na bodybuilding so ninachoongea ni personal experience na observation kwa wengine.
 
Aisee... shughuli za kunitoa jasho Ni chache Sana.... Hivyo nakua sedentary muda mwingi
Sedentary lifestyle pia ndio iliniletea kitambi. Kilianzia chuo, asubuhi nakula roast ya maini, mandazi au chapati kisha natuama tu mda mwingi kwenye laptop na jf😎😎😎 kwisha habari yangu.
 
Kwa kweli uzi bila picha ni sawa na kunywa baltika ukitarajia ikupe stimu za chui lite [emoji28][emoji28][emoji28]!!! Tuma kitambi hicho tuone tunaanzia wapi
Picha ya kitambi mkuu haitokusaidia
 
Back
Top Bottom