hongera kwa kuwa mstahimilivu na kaza mkuu, mi sikupi pole.
Kuna wakati unatakiwa kuweka vyeti ndani, na kuomba kazi ya ujumla, mfano
*juzi kati red cross walitangaza nafasi, ile ilikuwa fursa tosha maana kuna nafasi hazihijaji vigezo vya kitaaluma sana.
*restaurants nyingi wafanyakazi wanasumbua sumbua, tumia hiyo nafasi kuomba kazi popote hata kuhudumia wateja, baadaye haohao wateja wanaweza kuwa chanzo cha wewe kupata deal jingine.
*mtaani kuna vikundi vya vijana vilivyosajiliwa na vinakopesheka, unaweza tafuta kimoja ujiunge kama njia ya kutokea.
*badala ya kuchat sana mtandaoni, tumia mda kupitia sites za ajira,bila shaka unazifahamu mbili tatu kila baada ya siku kadhaa kuona updates.
* jifunze taaluma mpya kila siku ukiwa free kwa kutembelea workshops tofautitofauti za watu na kujenga nao urafiki.
hasta la vista[emoji123][emoji123]