Jinsi ya kuondoa msongo wa mawazo

Nashukuru mkuu
 
Nashukuru sana mkuu talifanyia kazi hili
 
Kuna kitu binafsi kinanipa shida kwanini Biashara inaonekana ni kazi ya walioshindwa maisha!!
Mtu yoyote aidha aliajiriwa kastaafu au kafukuzwa kitu cha kwanza biashara hii ndio sababu watu wanashindwa biashara sababu ni hiyo

Ushauri wangu kwako....hapa mjini unatakiwa kukomaa bila kujali kazi gani unafanya muhimu uwe na malengo kwamba hii kazi ninayofanya ni kama daraja kunifikisha ninakotaka kwenda
watu wengi wanakwama hata akipata kibarua kidogo anaoa mwisho maisha yanakufa kabisa
 
Duh nao n mtazamo
 
Hata dhahabu lazima ipitishwe kwenye moto ili ifae, usikate tamaa Ndugu yangu kama una leseni unaweza kutafuta mtu mwenye uber uendeshe nimeona matangazo mengi watu wanahitaji madereva. Kupata kazi siku hizi ni mchakato mkuu ila Amini Mungu ni wa kwetu sote na zamu yako inakuja.
 
Pole sana..ila usichoke kutuma maombi ya Kazi ipo siku yako tu Mungu atatenda
 
Mkuu nina bachelor of taxation from institute of finance management (2014)

Pia nguvu za kutosha kufanya kazi yoyote ile na eneo lolote lile kwa uwezo wote

Uzuri sichagui kazi kabisa
Pia ni mwaminifu na mchapakazia
Hebu ch kukusaidia nenda tawi lolote la bancAbc walizitqngaza nafasi za DSA wanachukua tu mtu yoyote wakiona anafaa kwa kuwa busy kwanza ili akili isipate kutu na kuongeza uzoefu na kazi yao ni kuziuza product zao na kwa kuwa wanatangaza na internal vacancy kwa kuwa wametanua matawi dodona na mwanza basi itakua rahisi kupata ajira ya kudumu,hiyo DSA mshahara wako ni namna unavyouza hizio account so kambi popote anza mdomdo....maana kila aliefanikiwa asilimia kubwa wamepitia changamoto nyingi
 
Mkuu ngoja niende sasa hivi nalifahamu tawi lao pale posta ngoja nipeleke cv leo leo mana kila kitu kipo

Takupa mrejesho mkuu
 
Mkuu ngoja niende sasa hivi nalifahamu tawi lao pale posta ngoja nipeleke cv leo leo mana kila kitu kipo

Takupa mrejesho mkuu
Sawa fanya hivyo,na uzuri product zao zinauzika sana hasa prepaid card....ukifanikiwa useme....pia angalia nafasi walizotangaza maana kuna matawi mapya dodoma na mwanza bancAbc
 
Nakushangaa eti msomi mwenye cv! rugha yenyewe uliyotumia kwenye uzi huu ina makosa kibao! Kilimo kinalipa sana na hasa kama unayo elimu yako bhana, njoo huku Kijijini mambo ni poa tu.
 
Hata we pia umetumia alama ya mshangao wakati haikutakiwa hapo(!) Ila kikubwa ni kuelewa

Anyway nashukuru kwa ushauri mkuu
Nakushangaa eti msomi mwenye cv! rugha yenyewe uliyotumia kwenye uzi huu ina makosa kibao! Kilimo kinalipa sana na hasa kama unayo elimu yako bhana, njoo huku Kijijini mambo ni poa tu.
 
Nakushangaa eti msomi mwenye cv! rugha yenyewe uliyotumia kwenye uzi huu ina makosa kibao! Kilimo kinalipa sana na hasa kama unayo elimu yako bhana, njoo huku Kijijini mambo ni poa tu.
Rugha Lugha
 
Ajira zimekua ngumu sana ndg,wengi hutumia mbinu ya kuomba internship na wakikubaliwa huwa wanapiga kazi hatari yan wanaonesha juhudi zote ktk utendaji kazi wao mpaka boss anashawishika kuwaajiri. ishu hapo ni kwamba hiyo pesa ya kwendea huko ofsini kufiga internship itatoka wapi, hapo ndo kasheshe mana maboss wengine wanaweza wakakukaushia hata miezi hawakuajiri mpaka mwenyewe unaamua tu kuondoka. Usikate tamaa ndg,endelea kupambana one day yes
 
Nakushangaa eti msomi mwenye cv! rugha yenyewe uliyotumia kwenye uzi huu ina makosa kibao! Kilimo kinalipa sana na hasa kama unayo elimu yako bhana, njoo huku Kijijini mambo ni poa tu.
Wewe mkosoaji mwenyewe umeandika upupu rugha=lugha , jf kila mtu mjuaji/msomi sasa kama huna cha kumshauri ungekaa kimya tu,sio kukosoa halafu we mwenyewe dishi limepoteza network
 
Wewe mkosoaji mwenyewe umeandika upupu rugha=lugha , jf kila mtu mjuaji/msomi sasa kama huna cha kumshauri ungekaa kimya tu,sio kukosoa halafu we mwenyewe dishi limepoteza network
Mkuu haya mambo sio ya kuchukulia serious watu tuko tofauti sana
 
Nakushangaa eti msomi mwenye cv! rugha yenyewe uliyotumia kwenye uzi huu ina makosa kibao! Kilimo kinalipa sana na hasa kama unayo elimu yako bhana, njoo huku Kijijini mambo ni poa tu.
Huu ni wivu wa wazi wazi unauonesha kuhusu elimu ya jamaa. Wapo wenye PhD na wanakosea kuandika kama kawaida. Kumbuka jamaa hajaenda kusomea mambo ya uandishi wa habari huko chuoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…