Travis Walker
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 323
- 334
Habari vijana wenzangu natumai muko wazima na wenye afya njema. Siku ya leo nimeamua kuwaletea makala hii kuhusiana na utaalamu wa kuongea kwa ufasaha na kuwa na sauti shawishi wakati unapoongea. Ni kawaida kwa mwanadamu au kiumbe chochote chenye kutoa sauti kuweza kubadilisha sauti kwa kuashiria ishara fulani ili iwe kama ni alama kwa wanaosikia sauti hiyo. Na ndio maana hata tunapolia huwa sauti zinabadilika ili kuashiria huzuni na maumivu. Sifa moja kubwa ya muongeaji ni kuwafanya unaongea nao kukusikiliza na kupenda maongezi yako na hii inatokana na jinsi unavyoongea. Leo nitakufahamisha jinsi ya kuongea vizuri ili watu waweze kukusikiliza. Nimekuja na hatua kadhaa zitazokuelekeza kufanya zoezi hilo kwa umakini.
1.KUJITAMBUA
Unajua hapa duniani tupo watu wengi na wa aina tofauti, kuna watu ni wenye akili nyingi huitwa high- inteligence na kuna watu wa kawaida ambao normal-brain. kuna utofauti katika makundi mawili haya. Watu wenye akili nyingi ubongo wao hufanya kazi kwa haraka zaidi na watu wa kawaida huwa ubongo wao haufanyi kazi haraka. Kwa watu wenye akili nyingi inakuwa vigumu sana kuelekeza maneno vizuri na kuweza kuongea kwa ufasaha kutokana na utendaji kazi wa haraka wa ubongo yao. Lakini watu wa kawaida inakuwa rahisi kufanya zoezi hili. Sasa ukijikuta unaongea kwa haraka unatakiwa uchukue mazoezi ya kujifunza kuongea kidogo kidogo.
2.KUELEWA UNACHOKIONGEA
Moja kati ya nyenzo madhubuti za kukufanya kuongea vizuri ni kuelewa vyema unachokiongea. Kama unashindwa kutoa ufafanuzi mzuri na maelezo yaliyonyooka basi kuongea fasaha inakuwa vigumu mno.Sasa ili uongee vyema unatakiwa kufahamu nini unachoongea.
3. KUANDAA SAUTI YAKO
Unapotaka kuongea mbele ya watu unatakiwa kuiandaa sauti katika mvuto. Sauti nzuri ya kuongea ni yenye gonda kwa mbali iwe nyororo halafu iwe inatokea kifuani na pia iwe inasikika vizuri.
4. ONDOA STRESS NA WASIWASI
Unapotaka kuongea unatakiwa kuondoa stress na wasiwasi , mbini nzuri hapa ni kujitengenezea mazingira ya kuhisi upo peke yako wakati unapoongea kuna watu wengi sana. Unapoongea unatakiwa kutazama wanaokusikiliza ili ukimbize khofu na watu hisia inao-endana na mazungumzo yako.
5.USIONGE KWA HARAKA
Kuongea kwa hararka kunaweza kusababisha kutonyoosha maneno vizuri na kukupelekea ugumu katika maongezi pia kunaweza kusababisha kushindwa kuongelea kile unachohitaji na badala yake kuongea mambo yasiyoeleweka
6.CHANGANYA TABASAMU
Unapoongea changanya maongezi yako na tabasamu pamoja na furaha na wala usiwaoneshe wanaokusikusikiliza wahaka na stress ulizonazo