Jinsi ya kuongeza mauzo

echuma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2010
Posts
311
Reaction score
80
wafanyabiashara wengi hufikiria kinachoongeza mauzo ni ubora wa bidhaa zao lakini kinachoongeza mauzo ni ubora wa bidhaa zako kwenye kichwa cha mteja wako,na ubora huo huchangiwa na brand yako iko katika nafasi gani kwenye soko

kuna aina nne za brand ambazo zikiimarika zote mauzo yatapanda kwa kasi japo kila unapokamilisha moja utakuwa unaona mabadiliko aina hizo ni
brand ya bidhaa,brand ya kampuni/ofisi,brand ya wewe mwenyewe na brand ya alama

karibu legacy impresion tukufanyie brand na kukufundisha pia kuhusu branding 0713603699
 
kila mtu anaweza kuwa mjasiriamali ila kinachotofautisha ni uwezo wa kukabiliana na matatizo na kuyatatua kwa muda elimu ya kitu unachofanya ni muhmu kwa ajili ya maendeleo yako
 
Mkuu Hapo sijakupata kabisa, hizo aina nne za brand zinakuja vipi? Hebu Chukulia mfano wa Kampuni ya SONY, Hawa jamaa brand name yao ni SONY na vilevile company name yao ni SONY, na ukija kwa Tanzania mfano Maji ya Kilimanjaro ni Brand Name na Jina la Kampuni ni IPP kama sikosei, sasa hebu tupe mfano mmoja hapo kwenye Kilimanjaro hizo brand nne ziko wapi? au Mengi naye ni Brand? kwa saababu hata mengi akifa bado Brand yake itaendelea kufanya viziri tu,

Na ishu nyingine ni kwamba kujenga brand name si ishu ya kitoto hata kidogo, na si swala la kuhudhuria semina, kuna hitajika vitu vingi sana mpaka kuja kujenga Strong brand, na Capital ikiwa ndo kitu namba moja makampun i mengi imewachukua miaka mingi sana mpaka kuja kujenga strong Brand name,
 
asante hata sony kuna sony vaio,sony wega,sony erickson nikiwa namaanisha sony ni jina la kampuni na sonyerickson ni jina la brand. Na kuhusu kilimanjaro kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ni maana ya brand,brand ni jina lolote halisi haijalishi ni la kitu vikundi au kampuni ambalo linatamkwa kwa herufi kubwa hii inamaanisha sio kila jina ni brand.
Kilimanjaro ni brand na inawakilisha vitu vitatu (mkoa,mlima na kampuni ya kusambaza maji) japo kuwa inatumika hvy lakini vyote vinanafasi yake na aina yake hivyo kila brand inajisimamia
Nguvu ya brand inategemea uwezo wa kuchukua na kutumia tabia

ni kweli brand inakusanya vitu vingi lakini iwapo ukiwa na elimu yake itakusaidia hata katika uendeshaji wako wa biashara yako kuna watu wengi wanahisi kufanikiwa ni capital na wanahc mauzo ni ubora wa product lakini ukweli ni kwamba kuna vingi mfano mtandao wa tigo ni mtandao ambao unamatatizo mengi ya kiufundi na kila siku wanaurekebisha lakini kwanini watu hawauhami na kwenda mitandao mingine kwa kasi?,hii inatokana na jinsi walivyojibrand ukianza na product wanajitahidi kuja na ofa mpya kwa kuangalia wapi ni wateja wao na wanataka nini nk,ukiangalia alama hapo wanajitahdi kuirudisha alama yao itambulike kwa mtandao wao tu na sio kwa maana nyingine ndio maana sasa hivi matangazo yao hawaitumii sana nembo ya ile o inayofanya kama inakonyeza wanatumia ile ya moja kwa moja,brand ikitumika kwa vitu vingi kwa wakati mmoja inapoteza uhalisia mfano yebo yebo ilikuja kama energy drink lakini ikatumika kwenye vitu vingi hadi ikapoteza uhalisia leo hii hakuna anaekumbuka kama ilikuwa ni energy drink kila mtu anamaana yake kanda mbili,aina ya kusuka,timu ya mpira,aina ya nguo n.k

hivyo elimu ya ujasiriamali bila elimu ya branding ni sawa na kutembea gizani huku umefumba macho.

Natumaini umenipata sasa mkuu na sisi tunatoa elimu na kufanya brand ya alama mkuu
 
Mkuu rand inajengwakatika mambo mengi sana a hakunaahali unaweza kujenga Brand kwa semina, na Brand inajenga ni pamoja na Quality na ulivyo ji postion katika soko so sijui mnato Elimu gani kuhusu rand kwa sababu mimi naweza anzisha kiwandacha Maziwa na nikawa nayaita CHASHA, nahapo tiyali hiyo ni Brn name yangu so kuanzia hapo watu watweza kujua CHASHA na the more nitakavyo strigle katika Ubora, Advatisment, distribution nakazalika ndo the more nitakavyo jenga Brand yangu
 
soma vizuri nilivyoelezea hapo juu kuhusu sisi na tunachofanya na brand inavipengele vingi ila vipo katika makundi manne brand ya mtu mwenyewe,brand ya bidhaa,brand ya kikundi au kampuni na brand ya alama ndio nikakupa na mfano wa mtandao wa tigo. Hata hlo sasha bila kulibrand haliwezi kuwa brand hadi uviunganishe vyote ndio unakuwa na brand bora kuna makampuni mengi lakini sio kila kampuni ni brand ndio maana nikakuandika brand ni jina lakini sio kila jina ni brand
 
mkuu kumbuka kuna kampuni kama general tyre alijaribu kufanya branding ya matairi ya michelini walijaribu lakini walipungukiwa na bundle ya full branding wakajikuta wametumia nguvu nyingi kwenye mteremko ilipofika wakati wa kupanda wakawa wameisha choka ikafeli.

hivyo branding ni kwa yeyote na sehemu yoyote na ili ufanikiwe ni lazima ufanye brand hata wewe mwenyewe mkuu usipofanya brand nzuri ya jina lako hauwezi kufanikiwa, hii ndio inawapata hata wasanii wetu wengi hapa mjini wanatafuta majina bila kujibrand hilo jina wakilipata watalifanyia nini na litawafaidisha vipi mwishowe wanaishia kuwa ombaomba mjini.

Brand huenda sambamba na masoko katika kampuni ndio maana Kutafuta masoko ni kujenga brand kwenye ubongo wa mteja unaemtegemea.
 


package nuzuri, nafuu na yenye manufaa kwa brand yako karibu sasa
wateja 10 wa mwanzo semina ya brand itatolewa bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…