asante hata sony kuna sony vaio,sony wega,sony erickson nikiwa namaanisha sony ni jina la kampuni na sonyerickson ni jina la brand. Na kuhusu kilimanjaro kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ni maana ya brand,brand ni jina lolote halisi haijalishi ni la kitu vikundi au kampuni ambalo linatamkwa kwa herufi kubwa hii inamaanisha sio kila jina ni brand.
Kilimanjaro ni brand na inawakilisha vitu vitatu (mkoa,mlima na kampuni ya kusambaza maji) japo kuwa inatumika hvy lakini vyote vinanafasi yake na aina yake hivyo kila brand inajisimamia
Nguvu ya brand inategemea uwezo wa kuchukua na kutumia tabia
ni kweli brand inakusanya vitu vingi lakini iwapo ukiwa na elimu yake itakusaidia hata katika uendeshaji wako wa biashara yako kuna watu wengi wanahisi kufanikiwa ni capital na wanahc mauzo ni ubora wa product lakini ukweli ni kwamba kuna vingi mfano mtandao wa tigo ni mtandao ambao unamatatizo mengi ya kiufundi na kila siku wanaurekebisha lakini kwanini watu hawauhami na kwenda mitandao mingine kwa kasi?,hii inatokana na jinsi walivyojibrand ukianza na product wanajitahidi kuja na ofa mpya kwa kuangalia wapi ni wateja wao na wanataka nini nk,ukiangalia alama hapo wanajitahdi kuirudisha alama yao itambulike kwa mtandao wao tu na sio kwa maana nyingine ndio maana sasa hivi matangazo yao hawaitumii sana nembo ya ile o inayofanya kama inakonyeza wanatumia ile ya moja kwa moja,brand ikitumika kwa vitu vingi kwa wakati mmoja inapoteza uhalisia mfano yebo yebo ilikuja kama energy drink lakini ikatumika kwenye vitu vingi hadi ikapoteza uhalisia leo hii hakuna anaekumbuka kama ilikuwa ni energy drink kila mtu anamaana yake kanda mbili,aina ya kusuka,timu ya mpira,aina ya nguo n.k
hivyo elimu ya ujasiriamali bila elimu ya branding ni sawa na kutembea gizani huku umefumba macho.
Natumaini umenipata sasa mkuu na sisi tunatoa elimu na kufanya brand ya alama mkuu