Jinsi ya kupangalia chumba cha kulala kiwe na mvuto zaidi


Need we say more? Asha D amekupa ushauri wa kitaalamu sana. Big up Asha D. Kumbuka TV iwe HD or Full HD, kunako coffee table weza magazine za ukweli chache tu kama vile Bang, Mens health na refrigerator/deep freezer etc.
 
Need we say more? Asha D amekupa ushauri wa kitaalamu sana. Big up Asha D. Kumbuka TV iwe HD or Full HD, kunako coffee table weza magazine za ukweli chache tu kama vile Bang, Mens health na refrigerator/deep freezer etc.

Mkuu ili kumaitain status kuna umuhimu wa TV kuwa 3D. Hiyo ndio teknologia ya sasa. HD imepitwa na wakati. sijui nisuggest kuwepo pia na sauna?
 
Hivi besti uliniambia unafundisha chuo gani vile lol!
 
Dena Hamisi yaan wewe ni chenga sana mkuu...chenga kwel kwel kama za kwenye coldrill,yeye anataka gheto liwe la kisasa katika mpangilio wenye mvuto ndo maana akawaomba wataalam kama Asha wakampa maujanja...

Nadhani wakati mwingine sio lazima kila thread uchangie ukiona hii imenikalia kushoto unawaachia wengine...do what you can and let others do what you cant do
 


Tulia Baba!!, weka kitanda cha kawaida, meza(coffee table), Friji, Cooker.......yaani vitu kawaida, kwani hawa wenzetu, si rahisi kualewa, atakuja oohh curtain mbaya, meza hiiii apana, kitanda...(Hawa wenzetu si rahisi kuwaelewa!!!!!)
 
Unajipigia promo utunase tusio na bondi.
 
mmmhhh nambie mpenzi huyo 'perfect wife' yukoje dear na sisi tumfuate?

Natengua kauli inakua; an almost perfect house wife...LOL .... nimeona nimejitega na nimegundua nisijechemka but enways ngoja ni PM the qualities.... Usisahau kutembelea album yangu, particularly hiyo ya interior designs...
 
Chumba cha kulala ni mahali ambapo unapatumia wakati ukiwa umechoka na unahitaji utulivu na pumziko.

Ni mahali ambapo unahitaji kuondoa stress zote na kutuliza mwili na akili, vilevile ni mahali ambapo kwa wewe uliyeolewa unapata faragha ya kutosha kuwa na mume wako.

Kutokana na umuhimu wa chumba cha kulala basi ni vyema kikawa na mvuto utakaokufanya ujisikie vyema kuwa ndani yake namuonekano wake uchangie katika kukuondolea uchovu na stress.

Haipendezi kuona chumba kikiwa kimejaa makaratasi, magazeti na vitabu kila mahali bila mpangilio mzuri.

Weka vitabu na makaratasi yote mahali pamoja na kama unaweza kupata kabati na ukaviweka humo ili chumba kionekane nadhifu na sio kiwe kama maktaba.

Nguo ziwe zimepangwa vizuri kabatini au sandukuni na zile chafu zikae mahali pake kwenye kapu la nguo chafu. Usiache nguo zinaninginia kila mahali kwenye milango, madirisha, besele n.k maana inafanya chumba kiwe kimejaa na kuondoa mvuto.

Chumba cha kulala sio stoo hivyo haipendezi kuhifadhi vitu vya zamani chumbani kama viatu visivyovaliwa, nguo za watoto zisizovaliwa, miavuli, makoti ya mvua, toys za watoto n.k kama kuna ulazima wa kuhifadhi vitu hivi chumbani basi tafuta sanduku la bati na uviweke na kuhifadhi juu ya kabati au mvunguni ili kuondoa mlundikano wa vitu chumbani.

Kipambe chumba chako kwa maua na mapazia ya kuvutia. usipambe tu sebule na jikoni na kusahau chumba cha kulala.

Chumba kinaongezeka mvuto pale unapokipamba kwa maua na vessel nzuri, fremu za picha, mapazia mazuri na pia kapeti zuri la kuvutia. Unaweza weka picha yenu mkiwa honeymoon kwenye fremu na kuiweka mezani au ukutani na ikawa pambo zuri sana la chumbani kwenu.

Wekeza kenye mashuka mazuri na yenye kuvutia. Mashuka mazuri yanakufanya ujisikie vizuri unapokuwa chumbani na vilevile unapokuwa umelala.

Hakikisha unayafanyia usafi mara kwa mara na kuyabadilisha badilisha sio kila siku mashuka hayo hayo (kauka nikuvae). Wewe pia ni pambo mojawapo la chumba, hakikisha unakuwa na nguo nzuri za kulalia zenye kuvutia na kukufanya ujisikie vizuri na mwenye kuvutia.

Hasa kwa wale walioolewa ni vyema kuzingatia hili na kuepuka kuvaa ma-tsheti ya zamani na madela kila siku unapoenda kulala au unapokuwa umejipumzisha chumbani.

E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
 
Mkuu umetoa darasa zuri sana kwa wote, wanawake na wanaume. Ni vema tukalielewa hili mwa mapana na marefu yake.
 
Sio tu chumbani sio stoo, bali sio museum! Asante kwa kutukumbusha.
Unafanya kazi za internal decor mkuu? Ungetufahamisha huenda huduma ikahitajika.
 
OK, umetoa somo zuri! shukrani za dhati kwako mkuu! endelea kutukumbusha na mengine yenye faida kama hili.
 
This is a "super" class! Jf is more than a Social University. Thanks YM, keep it up!
 
Tafuta ile picha ya mtoto wa makamba uone chumba cha kulala kinakuwaje. unatuuliza sisi wa kwa Mtogole hayo tutayajuaje.
 
Mh. Mabwepande na kwa mfuga Mbwa na room ya hivyo sina hakika. Hii Srade itakua na matumizi.

Bt Masaki, Obey, Mbezi, na kufananako na huko hii Srade inamatumizi .
Vinginevyo ina mpangilio mtamu! Nimeipenda .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…