Najua asilimia kubwa ya Watanzania hapa nchini wanaishi kwenye Nyumba za kawaida, nyingi zinakuwa na vyumba kuanzia 2 - 4, pia vyumba hvyo vinakuwa ni vidogo kwamaana kwamba havitoshelezi mahitaji yetu. Watu wengi sana wanatamani kuweka vitu vizuri katika nyumba zao lakini wanakosa nafasi.
Sasa leo nakuletea picha ambazo zinaweza kukusaidia kupangilia vitu vingi katika chumba kidogo.
*Nyumba nyingi zinakuwa na muhonekano kama huu;
View attachment 509675
View attachment 509676View attachment 509677
* Tuanzie sebuleni;
-Sebule nyingi kama unavyoziona zinaonekana zina mashelf mengi, hii ni kwasababu yakuweka vitu vidogo vidogo kama vile vitabu na viurembo vingine pia hata glass za wine na whisky.
*Pia kama sebule yako ni ndogo zaidi, unaweza tumia coffee table zenye drawers kama hizi;
*Kwa upande wa chumba cha kulala unaweza pangilia chumba chako namna hii;
hii inawafaa sana wanandoa au couples.
Kwa upande wa wanafunzi au wafanyakazi wa ofisini unaweza pangilia hivi;
Pia kama chumbani kwako hakuna nafasi ya kutosha kuweza kuweka kabati la nguo, jaribu kununua kitanda chenye drawers ili uweze kuweka mashuka, blanketi na baadhi ya nguo zako hata vitabu.
*Kwa upande wa toilet and bathroom unaweza iga hii hapa;
kama unavyoona mabafu mengi yameungana na choo, pia kuna drawers chache kwa ajili ya kuhifadhi mataulo.