Kwa utaratibu uliopo sasa hivi wa kutoa leseni, ukitoa RUSHWA hilo linakuwa ni tatizo lako mwenyewe!
kuna baadhi ya watanzania ambao wameshajenga tabia fulani kuwa bila "Middle man (mtu wa kati)" hawawezi kufanikisha mambo yao. wengi wao ndio wanaojipendekeza na vijiela vyao hata bila kuombwa rushwa!
Binafsi nilipata yangu hivi karibuni nililipa pesa halali na kufuata taratibu na bado nikapata ndani ya wakati,
cha ajabu nilikutana na baadhi ya watu wananishauri nitoe rushwa nishugulikiwa haraka, nikawambia sitoi.
Tusilaumu mamlaka usika, tujilaumu sisi tulioweka vijiela vyetu mbele kutafuta favour ambayo kimsingi inapaswa kuwa Haki yako! Kila mtanzania akisema NO kwa Rushwa-inakwisha tu!
Mind set change is very important!
Sehemu nyingi sana nimefanikisha mambo yangu kwa wakati na bila rushwa, lakini wengine wakienda kwa shughuli kama hizohizo, lazima walalamike kuwa wametokwa pesa isivo halali..WHY?? hii ni sawa na mwanamke anayejilengesha akishatongozwa analaumu wanaume waliomtongoza wakati alitengeneza mazingira yeye mwenyewe!
Watanzania tuache uzushi, na kulaumulaumu tu!