Dr. Zaganza
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 1,814
- 2,738
Kuku wa Asili ni wale ambao wamekuwepo hapa nchini kwa miaka mingi na damu yao haijachanganyika na ya kuku wa kigeni. Kuku hawa wana rangi na maumbo mbali mbali. Idadi ya kuku wa Asili hapa Tanzania inakadiriwa kufikia milioni 56. Kati ya kaya milioni 3.8 zinazojishughulisha na kilimo nchini, kaya milioni 2.3 hujishughulisha na ufugaji wa kuku wa asili. Kwa kawaida ufugaji wa kuku wa Asili hapa nchini kwetu Tanzania hufanywa na wafugaji wadogo wadogo wanaoishi kando kando ya miji na wale wanaoishi vijijini.
Kuku hawa hufugwa huria (freerange), yaani hufungiwa ndani nyakati za usiku na hufunguliwa asubuhi ili wajitafutie chakula. Kuku hawa hutoa mazao machache sana yaani nyama na mayai, kwa mfano kuku mmoja hutaga kiasi cha mayai 40-60 kwa mwaka badala ya 100-150 iwapo atatunzwa vizuri. Pia uzito wa kuku hai ni wa chini sana, wastani wa kilo 1.0–1.5 katika umri wa zaidi ya miezi 6 badala ya kilo 1.8–2.5 iwapo atatunzwa vizuri. Sifa za Kuku wa Asili: Wastahimilivu wa magonjwa, lakini ni muhimu wakikingwa na baadhi ya magonjwa ya kuku kama mdondo, ndui ya kuku nk. ili kuweza kuwaendeleza. Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini, lakini ili kuwaendeleza ni lazima kuwapa chakula bora cha ziada.
Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa, kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira magumu (ukame, baridi nk). Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa. Kwa kiasi fulani wana uwezo wa kujilinda na maadui kama vile mwewe. Pamoja na sifa hizi ni muhimu kuku hao wakapewa matunzo mazuri, wawekwe kwenye mabanda mazuri na imara, pia wapewe maji na chakula cha kutosha.
Kwa ushauri wa BURE juu ya;
1.Mbinu za kuzalisha kuku wengi kwa muda mfupi
2.Kuwafanya kuku wengi kutotoa kwa wakati mmoja
3.Kuchagua mtetea anayeweza kuatamia mayai yasiyokuwa yake
4.Jinsi ya kutambua mayai yaliyo na mbegu na yasiyo na mbegu:
Wasiliana name kwa namba 0713-039875