Jinsi ya kupata leseni ya Uuzaji Bidhaa Jumla na Rejareja (Wholesale & Retail Trade)

Jinsi ya kupata leseni ya Uuzaji Bidhaa Jumla na Rejareja (Wholesale & Retail Trade)

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,811
Reaction score
3,888

​

1*owfl1BKcA5V_xRsuC2ECpg.png

1. Pata TIN Number kutoka TRA​

Hatua ya kwanza ni kuhakikisha unayo Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hii ndiyo nyaraka ya msingi inayothibitisha kuwa wewe ni mlipa kodi halali. Bila TIN, huwezi kuendelea na mchakato wa maombi ya leseni ya biashara.

2. Usajili wa Kampuni au Jina la Biashara​

Kama leseni unayoomba ni kwa jina la kampuni, lazima uwe na Cheti cha Usajili wa Kampuni kutoka BRELA. Kwa biashara binafsi, hakikisha umeisajili na una cheti halali cha usajili wa jina la biashara. (Tunakusaidia kusajili jina la biashara)

3. Mkataba wa Pango (kama umepanga eneo la biashara)​

Iwapo unafanya biashara kwenye eneo ulilopanga, utatakiwa kuambatanisha mkataba wa pango unaoonyesha makubaliano kati yako na mwenye mali. Hii husaidia mamlaka kujua umepata idhini ya kutumia eneo hilo kibiashara.

4. Tax Clearance Certificate kutoka TRA​


Unahitaji kupata Cheti cha Uthibitisho wa Mlipa Kodi (Tax Clearance Certificate) kutoka TRA. Hii inathibitisha kuwa huna deni la kodi na unafuata masharti ya ulipaji kodi.

5. Vyeti vya Kitaalamu (kwa huduma zinazohitaji vibali maalum)​


Kama biashara yako inahusu bidhaa au huduma zinazodhibitiwa na taasisi fulani, lazima uwe na vyeti vya kitaalamu. Mfano:

  • TCRA kwa huduma za mawasiliano
  • TBS kwa biashara ya chakula
  • EWURA kwa mafuta
  • TMDA kwa dawa
  • Vyeti vya taaluma kwa sheria, udaktari, au uhandisi.
Usipoteze muda kupanga foleni TRA au Halmashauri. Mimi na timu yangu ya Victoria Agency tutakusaidia kupata leseni yako ya Uuzaji Bidhaa Jumla na Rejareja kwa haraka zaidi, bila usumbufu, na ukiwa na uhakika kila kitu kimekamilika kisheria. Wasiliana nasi sasa ili tuanze mchakato wako mara moja! +255693880325
 
Back
Top Bottom