Naamini wanajamvi wazima, nianze kwa kusema maisha ya sasaivi ni magumu bila kuthubutu na kujitoa kwakeli autoki kwenye haya maisha
Niende kwenye mada, mimi ni mwanachuo wa mwaka wa pili ninamshukuru mungu nina boom ila nikifikiria maisha baada ya chuo kwakweli ni kitendawili maana mtaani sirahisi ata kidogo ila nashukuru mungu kunipa ufahamu kabla sijamaliza chuo nimefuatiria sana mada za jf na nimesoma vitabu kadhaa nakujifunza kwamba ujasiriamali ni jambo muhimu sana tena sana ila mtaji imekuwa changamoto sasa mimi ninataka nipambane na changamoto hii kabla sijamaliza kwa njia hizi mbili
1)Ni kupitia kuwekeza pesa zangu kidogokidogo kwa kila boom kama laki mbili ili nikimaliza chuo niwe tiari na mtaji kama wa minimum 1,200,000 ambayo nitaanza hustle zangu nikiingia mtaani.
::changamoto ya hii njia inaitaji kujitoa maana ina mauvivu kuvumilia kipindi cha miaka miwili kubana pesa kwakeli ihsani za mungu zinaitajika katika njia hii lakini kitu nilichokipata kwenye njia hii ni kuweka fedha fixed account ambapo ata ukipata tamaa uwezi Pata pesa zako
2) njia ya pili ni yakuizingusha fedha kupitia biashara yoyote ile ambapo itakuwa inadharisha kidogokidogo mpaka kufikia kimaliza chuo unakuwa na mtaji mkubwa ambao utaweza kupita ata wanjia ya kwanza
::changamoto ya njia hii ni kupata asara kwasabu kwenye biashara kuna asara na faida kwaiyo unaweza usiupate uwo mtaji kabisa arafu kingine ni kuchanganya masomo na biashara ambapo unaweza kosa kimoja wapo
Tushirikishane yepi njia nzuri kati ya hizo na kama kuna njia nyingine tujulishane kama kuna makosa ya kuchanganya herufi tuvumiliane
NB: ukiona ngumu kutengeneza mtaji wako leo jua maisha ni magumu kuliko kutengeneza uwo mtaji (ugumu wa maisha unaboa sikidogo)