Mimi nitakufundisha mkuu
Umenikumbusha mbali Sana wakati nakaa na bibi yangu alinifundisha
Kwanza tafuta konokono wazima wale wanaokaa migombani au sehemu zenye unyevuunyevu (chukua wa kutosha) kisha tafuta sufulia kubwa waweke then Tia maji waweke jikoni wafunike, mpaka watokote kabisa ukijiridhisha waepue wakiwa hawajapoa tafuta kitu chenye ncha Kali tumia kifaa hicho kutoa mnofu wa konokono kwenye Ganda lake, ukimaliza waoshe vizuri kama unataka kukaanga weka viungo kama nyama ya kawaida kisha weka mafuta jikoni tayari Kwa kukaanga au ukitaka unaweza kuendelea kama nyama ya kawaida
Note
Nyama ya konokono ni Tamu Sana na haina mfupa
Kama unaswali jingine niambie