Jinsi ya kupika maandazi matamu ya maziwa na hiriki

Aaliyyah

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2022
Posts
19,041
Reaction score
46,239
Natumaini mko salama Leo naomba niwaletee recipe ya maandazi matamu laini na yanayoweza kukaa hata wiki yakiwa Bado laini na matamu

Mahitaji
Ngano kilo moja
Sukari robo (utaigawa mara mbili)
Iriki iliyosagwa Kijiko kimoja
Maziwa ya maji nusu lita
Mafuta ya kupikia(pima kikombe Cha ml 250kwaajili ya kukandia)
Amira Kijiko kimoja
baking soda Kijiko kimoja

Hatua ya kwanza
Weka ngano Yako kwenye beseni bandika mafuta ya kula jikoni yakipata joto mimina kwenye ungawako Anza kuchanganya had uhakikishe kuwa mafuta na ngano vimechanganyika vizuri hii ni muhimu

Hatua ya pili
Baada ya mchanganyiko kuwa laini weka Amira,baking soda,iriki pamoja na sukari kwenye ngano changanya Tena Kisha miminia maziwa kidogo kidogo huku unakanda
Hakikisha mchanganyiko wako unakuwa mlaini kias usiwe mgumu Kanda had unga wako uone uko smooth funika acha uumuke

Hatua ya Tatu
Ngano ikiumuka Anza kukanda Tena Kwa dakika 2 tunaita kutoa hewa Kisha sukuma na kata vipande size upendayo Kisha funika Tena au acha Tena iumuke Tena kidogo
Hii hatua ya kuacha iumuke Tena ni muhimu Kwa matokeo mazuri

Hatua ya nne
Bandika chombo Cha kupikia mimina mafuta yakipata joto weka maandazi Yako Anza kupika Kwa moto wa wastani

Maandazi haya ni mazuri laini na matamu sana jinsi ya kuyatunza hakikisha unaweka kwenye chombo au mfuko yasikae wazi hapo yanaweza fika siku 5 yakiwa na uborawake
IMG_20221106_094136.jpg
IMG_20230123_165156.jpg
 
Natumaini mko salama Leo naomba niwaletee recipe ya maandazi matamu laini na yanayoweza kukaa hata wiki yakiwa Bado laini na matamu

Mahitaji
Ngano kilo moja
Sukari robo (utaigawa mara mbili)
Iriki iliyosagwa Kijiko kimoja
Maziwa ya maji nusu lita
Mafuta ya kupikia(pima kikombe Cha ml 250kwaajili ya kukandia)
Amira Kijiko kimoja
baking soda Kijiko kimoja

Hatua ya kwanza
Weka ngano Yako kwenye beseni bandika mafuta ya kula jikoni yakipata joto mimina kwenye ungawako Anza kuchanganya had uhakikishe kuwa mafuta na ngano vimechanganyika vizuri hii ni muhimu

Hatua ya pili
Baada ya mchanganyiko kuwa laini weka Amira,baking soda,iriki pamoja na sukari kwenye ngano changanya Tena Kisha miminia maziwa kidogo kidogo huku unakanda
Hakikisha mchanganyiko wako unakuwa mlaini kias usiwe mgumu Kanda had unga wako uone uko smooth funika acha uumuke

Hatua ya Tatu
Ngano ikiumuka Anza kukanda Tena Kwa dakika 2 tunaita kutoa hewa Kisha sukuma na kata vipande size upendayo Kisha funika Tena au acha Tena iumuke Tena kidogo
Hii hatua ya kuacha iumuke Tena ni muhimu Kwa matokeo mazuri

Hatua ya nne
Bandika chombo Cha kupikia mimina mafuta yakipata joto weka maandazi Yako Anza kupika Kwa moto wa wastani

Maandazi haya ni mazuri laini na matamu sana jinsi ya kuyatunza hakikisha unaweka kwenye chombo au mfuko yasikae wazi hapo yanaweza fika siku 5 yakiwa na uborawake View attachment 3093778View attachment 3093779
Njoo unipikie hii wikend basi
 
Back
Top Bottom