Jinsi ya kupika Macaroni

sacha

Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
76
Reaction score
11
Jaman mwenye kujua namna ya kupika macaron ya nyama ya kusaga..ama sphaghett anisaidie..maana napenda sana huu msosi ila cjawah kuupikaa....
 
kuna mapishi aina tofauti tofauti unaweza pika nyama yako ya kusaga then ukachemsha sphagetti zako ukala spageti na nyama pembeni.....

Au ukaiunga na kuitengeneza nyama ya kusaga na kutia macaroni yaliyokwisha chemshwa
 
mahitaji
macaroni/spaghetti
nyama ya kusaga
maji
nyanya(kama unapenda sio lazima)
karoti na hoho
kitunguu
royco (kama unapenda)
mi huweka tui zito la nazi wakati fulani(sio lazima lakini)
chumvi
pia pili pili manga kidogo kwa taste flani hv tamu!
NJIA
1.chemsha nyama ya kusaga ikauke maji ya kwanza,weka pembeni kisha
1.Bandika maji yakishachemka weka chumvi kidogo
2.kisha weka macaroni yasiive sana (ladha yake inakuwa bomba zaidi yakibaki na ile shape yake)
3.weka kwenye chujio yachuje maji yawe makavu
4. kaanga kwa sekunde tanokaroti zilizokatwa kwa urefu kama mlo wako ni spaghetti na za round kama mlo wako ni macaroni (ziweke kwenye mafuta kwa pamoja)
5.weka nyama ya kusaga changanya vizuri na viungo, weka royco kidogo
6.weka macaroni /spaghetti changanya tena(hakikisha kila rangi bado inaonekana ile like karoti,nyama,spaghetti au macaroni vyote vonekane (ladha ya huu mlo ni zile rangi za vilivyomo zinaita kimsingi)
7.weka pilipili manga changanya tena hapa weka pia hoho zilizokatwa kubwa kubwa
8.weka tui la nazi(unaweza kuwa umeshalichemsha pembeni ILA HAKIKISHA UNAPOCHEMSHA LISIKATIKE KOROGA MFULULIZO,MWIKO USITOKE KWENYE SUFURIA MPAKA LIMECHEMKA)
serve
unaweza kusave na chai ya maziwa au ya rangi au hata juice mwake!
halihitaji garnish kwa kweli labda kama una King'asti syndrome ya kutaka kachumbari mpka kwenye chai!
 
Last edited by a moderator:
Hahaha. Ulijuaje, macaroni hata spaghetti zaliwa na kachumbari tena yenye mayonnaise!
Pishi zuri sana hili shosti.
 

mkuu umenigusa kidogo hapa naomba unielekeze kidogo nilienda kwa mtu mmoja hivi sio mmatumbi anyway akanikaribisha sphaghet yenyewe yalikuwa yale makubwa makubwa sio vile vidogo kama minyoo hivi ndani mwake kulikuwa na ladha ya mayonnaise halafu pia ndani yake kulikuwa na kuku ana rangi ya brown aisee hichi chakula kilikuwa kitamu sana nimejitahidi na mimi nifanye hivyo nimeshindwa kabisa ebu nipe ujanja hapa hayo mayonnaise unayaweka wakati gani ili ilete ladha hiyo? na mimi ni mpenda pili pili je naweza kuweka ndani ya spagheti? halafu nipo kwa wamatumbi wenzangu suala la pilipili manga hawaijui hivi kwa lugha ya kitaalam inaitwaje mean in english? ili nikienda supermarket nisionekane kituko bure
 
UKI black pepper - pilipili manga.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: UKI
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…