Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mahitaji
macaroni/spaghetti
nyama ya kusaga
maji
nyanya(kama unapenda sio lazima)
karoti na hoho
kitunguu
royco (kama unapenda)
mi huweka tui zito la nazi wakati fulani(sio lazima lakini)
chumvi
pia pili pili manga kidogo kwa taste flani hv tamu!
NJIA
1.chemsha nyama ya kusaga ikauke maji ya kwanza,weka pembeni kisha
1.Bandika maji yakishachemka weka chumvi kidogo
2.kisha weka macaroni yasiive sana (ladha yake inakuwa bomba zaidi yakibaki na ile shape yake)
3.weka kwenye chujio yachuje maji yawe makavu
4. kaanga kwa sekunde tanokaroti zilizokatwa kwa urefu kama mlo wako ni spaghetti na za round kama mlo wako ni macaroni (ziweke kwenye mafuta kwa pamoja)
5.weka nyama ya kusaga changanya vizuri na viungo, weka royco kidogo
6.weka macaroni /spaghetti changanya tena(hakikisha kila rangi bado inaonekana ile like karoti,nyama,spaghetti au macaroni vyote vonekane (ladha ya huu mlo ni zile rangi za vilivyomo zinaita kimsingi)
7.weka pilipili manga changanya tena hapa weka pia hoho zilizokatwa kubwa kubwa
8.weka tui la nazi(unaweza kuwa umeshalichemsha pembeni ILA HAKIKISHA UNAPOCHEMSHA LISIKATIKE KOROGA MFULULIZO,MWIKO USITOKE KWENYE SUFURIA MPAKA LIMECHEMKA)
serve
unaweza kusave na chai ya maziwa au ya rangi au hata juice mwake!
halihitaji garnish kwa kweli labda kama una King'asti syndrome ya kutaka kachumbari mpka kwenye chai!