Jinsi ya kupika mayai aina tofauti

Jinsi ya kupika mayai aina tofauti

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
9,296
Reaction score
7,683
Omlette
Huu unakuwa mchanganyiko wa mayai,chumvi,pilipili manga,na mboga mboga ukipendelea kama kitunguu maji, pilipili hoho, nyanya n.k
  • Kaanga kitunguu na mafuta vijiko viwili vya supu kwanza mpaka kibadilike rangi kiwe hudhurungi kisha unakaanga na pilipili hoho kama dakika 5,mwisho unaweka mchanganyiko wa mayai na nyanya ilokatwakatwa,ukiwa unapendelea yai lisilo kavu unakuwa huhitaji kuligeuza ili liive na upande wa pili lakini hakikisha ule upande wa chini unaivisha upande wa juu kwa moto mdogo mpaka liwe creamy, Nyunyuizia cheese juu na kulikunja mara mbili.
omlette.jpeg
images.jpeg
images (1).jpeg
  • Unaweza kuweka na vitu vingine pia ukipendelea kama kombe/chaza,kamba,uyogan.k
  • Unaweza pia kukaanga viazi viwe slices na kitunguu maji kisha unanyunyuizia yai, linaitwa spanish potato egg tortilla(kikwetu chipsi mayai/zege).
chipsi mayai.jpeg

Hardboiled egg:
  • Hili ni yai la kuchemsha la kawaida,unalichemsha kwa dakika 10-15.
hard boiled egg.jpeg

Soft boiled egg:
  • Hili ni yai pia la kuchemsha lkn linakuwa na urojo mzito ndani.Yai hili huchemshwa dakika 3-4 ni muhimu kufata muda.
soft boiled gg.jpegsoft.jpeg

Poached egg:
  • Yai hili hupikwa kwa kuvunjiwa ndani ya maji. Injika sufuria pana na uweke maji 1/2 sufuria. Unaweza kutumia maziwa baadala ya maji kuongeza ladha.Ukiwa unatumia maji weka siki vijiko viwili au maji ya limau.Punguza moto ili maji yasichemke sana. Vunja yai kwenye bakuli na hakikisha hukiharibu kiini cha yai. Tumia kiijiko kikubwa koroga maji yafanye circulation kisha weka yai lilokuwa kwenye bakuli katikati ya hio circulation ya maji.Subiri dakika 3-5,yai likiiva linabadilika na kuwa jeupe kwenye ule ute.
poached 2.jpegpoached.jpeg

Scrambled egg:
  • Yai hili hupikwa kwa kupiga mayai kadhaa,na mchanganyiko wa chumvi,pilipili manga, maziwa/cream ukipendelea kuongeza ladha.Unaweza kutumia siagi au mafuta ya kawaida kukaangia.Mimina mchanganyiko wako,wacha kama dakika 2 kisha yavuruge mayai, kama unakoroga.Fanya hivo kwa dakika 3 nyingine.Epua kwa kuliwa
scrambled.jpeg

Sunny side-up/Macho:
  • Yai hili lina pikwa na kiini cha macho linakuwa na rojo.Weka mafuta yapate moto kama vijiko viwili vya supu.Vunjia mayai juu ya kikaangio hakikisha huharibu kiini.Nyunyuizia chumvi na pilipili manga.Waacha liive ule ute wa yai.
  • Ukipendelea unaweza kuligeuza ili lipate kama layer ya juu au kufunika ili ile layer ya juu iive na mvuke.
sunnyside-up.jpeg

French toast:
  • Hii ni slesi ya mkate ambao inachovya kwenye mayai yalopigwa na kukaangwa kwenye fryingpan ya mafuta kama unavyokaanga mayai ya kawaida.
french toast.jpeg

Bon appetitte 🙂
 
Wowwww mhhh ....halaf sometime tunaendaga restrnt unaletewa menu unaona vitu vya ajab kweli!! Thanks mimi49 kwa kutuekea upishi tofauti wa yai...halaf kuanzia sasa inabidi nijifunze na haya majina yaani huku kwetu likiwekwa kitunguu yai likipikwa lenyewe pia yai hatunaga jina lengine tunalotumia;-)
 
Last edited by a moderator:
Wowwww mhhh ....halaf sometime tunaendaga restrnt unaletewa menu unaona vitu vya ajab kweli!! Thanks mimi49 kwa kutuekea upishi tofauti wa yai...halaf kuanzia sasa inabidi nijifunze na haya majina yaani huku kwetu likiwekwa kitunguu yai likipikwa lenyewe pia yai hatunaga jina lengine tunalotumia;-)

Ha ha ha nakwambiaaaa...lkn itakuwa vyema yakitafutiwa majina ya kiswahili 😄
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom