Aaliyyah
JF-Expert Member
- Mar 20, 2022
- 19,041
- 46,239
Natumaini wazima.
Leo nawaletea recipe ya kupika samaki wa Nazi chukuchuku,wengine wanasema mchuzi ambao hauna mambo mengi
MAHITAJI
Samaki wabichi unaweza tumia pia wakavu.
Nazi, karoti, hoho, kitunguu maji, nyanya, chumvi na ndimu ukipenda.
Andaa viungo vyako katakata size utayopenda.
Unaweza kuongezea biringanya, bamia au nyanya chungu kama ukipenda
Weka kwenye sufuria samaki, nyanya, karoti, kitunguu maji na chumvi Kisha weka maji kidogo Ili kuivisha viungo pamoja na samaki zingatia kipimo Cha maji
Ukiona vimeiva weka Nazi kwenye mchuzi wako acha ichemke.
Hakikisha ugeuzi Wala kukoroga koroga sana unaweza ukawa unatumia njia ya kutikisa tu sufuria kidogo Ili mchanganyiko ukae vizuri ikiiva ipua tayar Kwa kula.
Unaweza kula na wali au ugali
Mimi sijatumia nyanya,nimetumia karot wewe unaweza amua kama unatumia bas zisiwe nyingi
Nazi sio lazima ya kukuna kama yangu mnaweza kutumia ya pakti 😍
Nawatakia siku njema