Jinsi ya kupika pilau na kuku wa kienyeji

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Wakati Shughuli nyingine za Kitaifa na Kimataifa zikiendelea tujitahidi kula vizuri ili tupate Nguvu zaidi ya kusikiliza na kutoa maoni katika baadhi ya mambo.

Lakini pia hata kama una madeni kiasi gani, una huzuni kiasi gani wewe usiache kula vizuri ili upate Nguvu ya kutatua hizo changamoto zako.

Turudi kwenye mada sasa ya Mapishi.

Mimi napenda kupika sana na nikikosea baadhi ya mambo naomba mnirekebishe taratibu.

Kila Mtu ana njia mbalimbali ya kupika na Chakula kuwa kizuri tu sana.

Wewe unapikaje Pilau Kuku wa Kienyeji?

Kwangu mimi lazima nifanye maandalizi kwanza kama ifuatavyo:-

Mahitaji
  • Kuku Mzima wa Kienyeji
  • Mchele Kilo moja
  • Viazi Mviringo Vinne
  • Tangawizi
  • Vitunguu Maji.
  • Vitunguu Saumu
  • Viungo vya Pilau.
  • Karoti
  • Hoho.
  • Mafuta ya kupikia.
  • Chumvi.
Maandalizi
Mtengeneze Kuku wako vizuri na katika hali ya Usafi Muwekee Kwenye Chombo Cha kupikia.

Mpake Viungo Ulivyokwisha Viandaa kama Tangawizi na Kitunguu Saumu.

Weka Chumvi, kisha Mbandike. Muda wa kuiva utategemea na ulaini au ugumu wa Kuku mwenyewe.

Kuku akiendelea Kuchemka unaweza kuendelea na maandalizi ya Vitu Vingine kama Mchele na Kutengeneza Viungo Vingine ili Kuku akiiva iwe rahisi kupika.

Hakikisha Nyama inabaki na mchuzi wake Baada ya Kuiva.

Bandika Sufuria lako kwa ajili ya kupika Pilau liwe na nafasi ya kutosha kwa sababu Nyama ya Kuku inakuwa na Vipande Vikubwa Vikubwa.

Weka Mafuta kwa kipimo kinachotosha, weka Vinguu Maji, Vipike Viive Vizuri hadi kuwa na rangi ya kahawia.

Baada ya hapo weka Tangawizi na Kitungu Saumu koroga vizuri, Weka Karoti, koroga vizuri hadi Viive.

Kisha weka mchanganyiko wa Viungo vyako vya pilau, koroga vizuri hadi viive vizuri.

Weka Viazi Vyako, kisha Kuku wako. Endelea kukoroga. Halafu hapa unaweza kuweka Ile Supu ya Kuku.

Utaacha uchemke kwa muda kidogo, kisha utaweka Mchele wako na kugeuza vizuri. Funika na kuacha pilau lako liive vizuri.

Pilau linafaa kupika kwa Jiko la Gesi, Umeme,Kuni na Mkaa. Pilau ni Chakula ambacho kinaliwa muda wowote Mchana au Jioni.

Unaweza kula kwa kutumia Juisi au Soda na hata Chai pia.
 
Attachments

  • 3EA5828A-D41F-4086-BABE-E592D7B5EEBF.jpeg
    3EA5828A-D41F-4086-BABE-E592D7B5EEBF.jpeg
    130.1 KB · Views: 29

Ushimen mpishi wako ni nyota tano eeh!
 
Back
Top Bottom