falcon mombasa
JF-Expert Member
- Mar 5, 2015
- 9,189
- 9,299
Mahitaji maziwa, mayai, sukari kidogo, hiriki.
Utayarishaji wake, pasua mayai kutokana na size ya chakula unachotaka kupika, yakoroge hadi yachanganyike vizuri, kisha anza kuchemsha maziwa ambayo tayari umeyachanganya na hiriki, yanapoanza kuchemka changanya mchanganyiko wa mayai kisha funika vizuri kama mtu anaeoka mkate.
Hakikisha moto sio mkali, acha mchanganyiko wako uchemke kwa dakika kumi.
Ukienda kufunua utakuta podini yako iko tayari katika umbo la keki au mkate wa kumimina, chini ya podini itakuwa imebadilika rangi kuwa kama kahawia.
Sasa unaweza kuiweka katika sahani, kisha chukua kisu na uma na uanze kukata podini yako vipande na uanze kufurahia chakula hiki kitamu cha asili ya Mombasa Kenya.