Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nipo farkhina nilikuwa kwenye shangwe za birthday yangu jana, japo nilitegemea bonge la keki toka kwako
nipo farkhina nilikuwa kwenye shangwe za birthday yangu jana, japo nilitegemea bonge la keki toka kwako
Owh happy birthday labda nimechelewa kuku wish....hope ulifurahia vizur
Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Angel alikua wap kwani ....yy ndo alikua aliteremshe bongezz la cake sote tupate vijipande...lol
alikuwepo na tulienjoy mno ila tukawish tutapata xtra from u farkhina our super chef
Nice subir niwaite
Mrs Kharusy BAK Ndetichi amu measkron gorgeousmimi Swts Ennie xiexie Kim nana Chocs Heaven on Earth mshana jr Angel Nylon Nyani Ngabu MziziMkavu
Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Nimetamani hilo pishi inabidi kesho nilipike
Kuna sehemu nililiona ili pishi nikajaribu kulipika aisee ni tamu asikwambie mtu, hii ni kwa wale wenzangu na mimi wanaopenda kujaribu jaribu mapishiii.
MAHITAJI
1: Mayai Manne.
2: Nyanya tatu.
3:kitunguu maji kimoja.
4😛ilipili hoho moja.
5: karoti moja.
6: nyanya chungu(KAMA UKIPENDA) tatu.
7: Nazi moja. 8: Mafuta ya kupikia chupa moja.
9: Chumvi upendavyo.
JINSI YA KUANDAA
1; Chemsha mayai yako kwa dakika 15, yakisha iva yaepue yaache yapoe halafu yamenye.
2; Weka mafuta ya kula kwenye moto wa wastani yakisha pata moto weka mayai yako ambao umeyamenya na yakapoa yaache mpaka yawe na rangi ya kahawia ila yasikaukeee halafu yaepue ili yajichuje mafuta.
4; katakata nyanya, karoti,nyanya chungu, kitunguu maji na pilipili hoho.
5: kuna nazi yako halafu chuja matui mawili kama unavyounga maharage.
6: weka sufuria jikoni weka na mafuta kidogo ya kuungia mboga halafu weka kitunguu maji kiache mpaka kiwe kahawia halafu weka karoti nazo kaanga mpaka zibadilike rangi kidogo halafu weka pilipili hoho kaanga kidogo halafu uweke nyanya na nyanya chungu halafu funika mpaka ziive kidogo (usisahau kuweka chumvi kwenye huo mchanganyiko).
7: mchuzi ukishaiva iva weka mayai yako ambayo ulishayakaanga halafu weka tui jepesi halafu piga piga mpaka liive(lichemke) likishaiva weka tui bubu nalo piga piga mpaka nalo liive (lichemke) likishaiva likisha iva epua.
Mboga yako ipo tayari kuliwa unaweza kula na kitu chochoteee. Karibuni.....
Mafuta ya kupikia chupa moja?! Are you serious?!