Angel Nylon
JF-Expert Member
- Jul 26, 2011
- 9,164
- 18,402
Mbona vinakuwa vigumu tofauti na vile vya mtaani vinakuwa lainii na sukari yake hadi raha sema vinavutika km mpira.
Msinichoke mpishi mm
Kuna visheti vya aina 2. Kuna hivyo vigumu, vinakua vidogo vidogo. Na kuna hivyo unosema ambavyo kavitaja farkhina hapo vya namba 8 au shape si lazima vinakua vikubwa kama doughnut hivyo hukandwa kwa nazi Na vinakuwa vilaini. Lkn katika uwekaji wa shira ni kama hivyo vidogo.
Mi sijui vinavopikwa maana tumezoea sana kununua. Hivyo vidogo ndo watu wengi wanapika nyumbani vya kutafuna Na kahawa jioni, jioni. Au hata kutoa sadaka kwa wtt au miskitini.
Last edited by a moderator:



