Airmanula
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 3,527
- 5,762
( Chakula hiki kinatosha watu 3 hadi 5 )
600 gram mchele wa basmati basmati
1 Kuku mzima ( toa ngozi na kata vipande vikubwa kama kwenye picha)
6 Vitunguu umbo la kati
15 Gram kitunguu swaumu cha kusagwa
10 Gram tangawizi ya kusagwa
3 Nyanya katakat vipande vidogo
3 Pili pili mbuzi za kijani
1 Fungu la majani ya Mint
1 Fungu la majani ya Coriander (giligilani)
3 Kijiko kidogo cha chai Garam masala
100 gram Yogurt
1 Kijiko kikubwa cha chakula juisi ya limao
3 Kijiko kikubwa cha chakula mafuta ya samli
3 Kijiko kikubwa cha chakula maziwa ya maji
Viungo vizima pia vinatakiwa
3 Vipande vya mdalasini cinnamon stick
6 Vipande vya karafuu
2 Vipande vya hiriki ya kijani
Kwa kupambia biriyani yako
Mafuta ya kukaangia
1 Kitunguu kata slice
10 Vipande vya korosho (Cashew nuts)
15 Vipande vya zabibu kavu (Rasins)
Jinsi ya kupika fatilia maelezo
1. Loweka mchele kwenye maji kwa masaa 3.
2. Kisha chemsha mchele katika maji, chumvi na 1 kijiko cha garam masala kwa dakika 15, kisha toa mchele wako uchuje na weka pembeni. Wali huu ukiubonyeza kwa mikono utavunjika ingawa utakua haujaiva vizuri. Huu ndio ubora unaotakiwa kwani ukiivisha kabisa utakua umekosea.
3. Safisha kuku na kata katika vipande vikubwa.Kumbuka kukata kata mikato katika nyama ili iweze kuja kuiva haraka.
4. Chukua sufuria kubwa linaloweza kuingia mchele na kuku yoote wakati unapika. kisha weka samli iyeyuke.
5. Kisha weka viungo vyoote na kaanga mapaka upate harufu nzuri (aroma).
6. Kisha weka kitunguu na chumvi. Pika mapaka vitunguu vilainike. Kisha punguza moto uwe wa wastani.
7. Kisha weka kitunguu swaumu na tangawizi kaanga mpaka upate rangi ya kahawia.
8. Kisha weka nyanya na pili pili mbuzi. Acha mchanganyiko huu uive mpaka nyanya ipondeke .
9. Kisha weka majani ya mint na coriander . Funika na mfuniko na pika kwa dakika 10.
10. Kisha weka yogurt na unga wa garam masala.
11. Kisha ongeza limao juice na chumvi kidogo.
12. Kisha chukua vipande vya kuku na weka katika mchanganyiko wako katika sufuria, funika na uache inaendelea kuiva.
13. Kisha chukau wali na weka juu ya mchanganyiko wako wa kuku na mchuzi.
14. Kisha mwagia maziwa juu ya wali.
15. Funika sufuri a yako hakikisha inafunika kabisa mvuke usitoke nje.
16. Baada ya hapo weka moto uwe mkali kabisa kwa dakika 2. KIsha punguza moto na acha ichemke kwa dakika 45.
17. Wakati huo huo pasha moto kikaango ili uweze kukaanga vitu utkavyopambia.
18. Choma vitunguu katika mafiuta mpaka upate rangi ya kahawia.
19. Kisha kaanga korosho mpaka rangi ya kahawia.
20. Kisha kaanga zabibu kavu kwa dakika 1 tu.
21. Baada ya kusubiri kwa dakika 45 sasa zungusha wali wako pamoja na nyama ya kuku vichanganyike pole pole.
22. Pakua chakula chako na ukipambe kisha mpatie mlaji kikiwa cha moto.
Endapo unataka kutumia nyama ya aina tofauti basi fanya haya
1.Kama unataka kutumia nyama ya ngombe au ya mbuzi au ya kondoo.
Unatakiwa nyama uiwekee viungo hivi na ikae usiku kucha katika friji ili iweze kua laini ( 100 gram yogurt, 1 kijiko cha chakula white vinegar- 1 kijiko cha chai garam masala powder).
Kwa mtindo huu wali itabidi upike kwa dakika 10 pembeni. Katika sufuria ya mchanganyiko wa nyama kwa kufata hatua zile ziule kitakachoongezeka ni muda wa kupika ikiwa ni nyama pika kwa saa 1 na dakika 15.
Mdau anahitaji kujua kuhusu upishi wa biriyani
Kwa wakazi wa mkoa wa Arusha ..wapi naweza kupata wali wa biriani mzuri na nyama nzuri either ya ngo'mbe au kuku.