Jinsi ya kupima ardhi yenye maji yanayotosha kwa kilimo ch umwagiliaji

Jinsi ya kupima ardhi yenye maji yanayotosha kwa kilimo ch umwagiliaji

WENYELE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,433
Reaction score
1,442
Natanguliza shukran zangu kwenu wataalam.
Mimi ni mhitimu kutoka Sua,na Mwenyeji wa Mkoa wa Simiyu wilaya mpya ya Itilima.
Nimepata kazi ya kuajiliwa lakini boss wangu kani-inspire sana koz yeye kafungua kampuni na kuajili watu huku akiwa still ni mwajiliwa na yeye.Kwa Elimu yangu ya kilimo niliyoipata kutoka SUA nami nimeamua nijibanebane na ka mshahara kangu halafu nianzishe kilimo cha umwagiliaji kijijini kwetu.Tatizo kubwa eneo tulilopo kijijin kwetu hakuna mto sasa nawaza kuchimba visima vireefu ili nipate maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Kwa hiyo basi nawomba wataalam wa water system and irrigation mnisaidie jinsi ya kupima ardhi yenye maji karibu ya kutosha kwa umwagiliaji.
Ahsante sana,Vijana kwa pamoja tunaweza.
 
Back
Top Bottom