Mkuu, ulikuwa utani tu mimi mlalahoi bin taabani mwenzako.
Twende kwenye mada, kujenga mwili na muonekano mzuri wa mwili kunahitaji kuzingatia kufanya mazoezi ya mwili kwa kujichanganya gym( kama ndio unaanza utasaidiwa na mtaalamu), pia ni muhimu kuzingatia ulaji wa mpangilio na kuepuka kula hovyo hovyo hapa namaanisha upate mlo kamili na wa kutosha.
Vyakula vya protini ndivyo unapaswa utumie kwa wingi sana badala ya vyakula vya wanga, bila kusahau unywaji wa maji ya kutosha pamoja na matunda na mbogamboga.
Ukizingatia hayo juu utaanza kuona mabadiliko ingawa inaweza ikachukua muda kuanza kuona mabadiliko.
Ukitaka mabadiliko ya haraka haraka kuna dawa( anabolic steroid- ni muhimu uwasiliane na daktari au mfamasia kabla ya kutumia) ambazo utapaswa kutumia ili uweze kubadilika kama wale body builders.