youngkato
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 3,811
- 3,888
Jinsi ya kusajili biashara yako ya Mtandaoni (Online Business)
Kama huwezi kuanza moja kwa moja na kampuni, usiogope anza na jina la biashara na mengine utamalizia kwa badae. Hapa chini kuna hatua kuu ambazo zitakuongoza ili usajili wako uwe rahisi, wa haraka na wa kisheria kabisa.Naamini unajua kwa nini ni muhimu kusajili biashara yako na faida unazoweza kupata baada ya kufanya hivyo. Usajili wa biashara ni njia ya kuongeza uaminifu wako, kinga ya mali zako, na fursa ya kukua kibiashara.
Hatua ya 1: Amua Aina ya Usajili
a. Chagua kama unataka jina la biashara, ubia, au kampuni.
Uamuzi huu utakusaidia kujua nyaraka zinazohitajika na gharama utakazokutana nazo.
Hata kama huanzi na kampuni, unaweza bado kupata leseni na namba ya mlipa kodi (TIN), ambavyo ni muhimu kwa kila mfanyabiashara.
Hatua ya 2: Ingia Tovuti ya BRELA
Usajili wa biashara hauhitaji tena foleni za ofisini unaweza kufanya kila kitu mtandaoni.
Fungua akaunti ya ORS, chagua huduma unayotaka (kampuni au jina la biashara), na ujaze taarifa zako zote: jina la biashara, umiliki, eneo na aina ya biashara.
Ukiwa tu na namba ya NIDA nitakusaidia kukamilisha kila kitu.
Hatua ya 3: Kamilisha Taratibu za Usajili
Lipa ada ya usajili mtandaoni na upate cheti cha usajili.
Ikiwa unasajili kampuni, utahitaji nyaraka za kisheria kama katiba ya kampuni na makubaliano ya wamiliki hizi hufanywa na mwanasheria.
Hatua ya 4: Pata Namba ya Mlipa Kodi (TIN)
Baada ya kusajili biashara, pata TIN yako moja kwa moja mtandaoni kupitia www.tra.go.tz au www.ots.tra.go.tz.
TIN inakuruhusu kulipa kodi kisheria na ni kosa kubwa kisheria kufanya biashara bila kulipa kodi. (Ukikwama nitakusaidia kuipata kwa haraka)
Hatua ya 5: Pata Leseni ya Biashara
Baada ya kupata TIN, tafuta leseni ya biashara kulingana na aina ya biashara yako:
Biashara ndogo na za rejareja: leseni zinapatikana kwenye halmashauri za manispaa au wilaya.
Biashara maalum kama viwanda, uchimbaji, au mikopo: leseni zinatolewa na wizara ya viwanda na biashara.
Baada ya kupata leseni, biashara yako inakuwa halali kabisa na inalindwa kisheria.
Umuhimu wa Kulinda Biashara Yako
Kufanya usajili peke yake hakutoshi — linda biashara yako dhidi ya majanga yasiyotarajiwa kama moto, wizi au majanga ya kiasili. Njia bora ni kupitia bima ya biashara:
Unapokata bima, unakuwa na uhakika kwamba ukipatwa na dharura, hutapoteza kila kitu.
Bima ni rahisi; hulipa michango midogo midogo na kulindwa dhidi ya hasara kubwa.
Mimi na timu yangu tutakusaidia kila hatua: kufanya usajili, kupata leseni, hadi kukuletea wateja kupitia mbinu za kisasa za masoko.
Tuma ujumbe WhatsApp sasa hivi 👉 +255693880325 na anza safari ya kufanikisha biashara yako haraka na kwa usahihi.