kuna faida gan kujisajili kama kampuni ukilinganisha na kusajili biashara.......kampuni inakuwa na sifa gani hasa
Mkuu maswali yako ni mafupi mafupi lakini ni mapana sana. Nami ntajitahidi kuyajibu kwa upana wake
1. Utangulizi
Kampuni ni asasi au shirika linalohusika kufanya biashara/shughuli nyingi kihalali
2. Aina za kampuni
a) Kampuni binafsi
Ni kampuni yenye ukomo ambayo wamiliki wanawajibika kisheria kwa kiasi cha mtaji walichowekeza tu
b) Kampuni tanzu
Ni kampuni yenye kumiliki nusu ya mali zinazomilikiwa na kampuni nyingine
c) Kampuni ya umma
Hii ni kampuni inayomilikiwa na serikali au inaweza kumilikiwa na serikali pamoja watu binafsi
===>Sifa za kampuni
Sifa za kampuni zinategemea na aina ya kampuni kama nilivyoainisha hapo juu. Sifa hizo ni kama ifuatavyo:
1. Kampuni binafsi
A. Inaundwa na watu wenye uhusiano wa kijamaa kabla. Mf baba na mama, baba na mtoto nk
B. Idadi ya wanahisa waundao kampuni ni kuanzia 2 na mwisho 50
C. Ina ugumu katika kuhamisha hisa hivyo ni ngumu kusajiliwa katika masoko ya hisa
2. Kampuni ya umma
A. Inaundwa na serikali na vilevile makampuni au watu wengine
B. Haina idadi kamili ya wamiliki
C. Ni rahisi kuhamisha hisa hivyo ni rahisi kuisajili soko la hisa
3. Kampuni tanzu
A. Ina umiliki wa kampuni nyingine ambayo inaweza kuwa nje ya Tanzania
===> Faida za kusajili kampuni dhidi ya jina la biashara ni kama ifuatavyo:
1. Mtaji
Mtaji kwa kampuni mnachanga hivyo inategemea uwezo wenu wa kuanza na mtaji kiasi gani na kuongezea kwa kuvhanga zaidi ya mtu watu wawili LAKINI katika suala la jina la biashara mtaji huwa kutoka kwa mmiliki mmoja tu hivyo uongezekaji wa mtaji unakuwa mgumu
2. Hadhi ya kisheria
Kampuni ina hadi kisheria kama asasi inayojitegemea hivyo hata panapotokea jambo basi kampuni ndiyo huhusika kisheria LAKINI jina la biashara jambo lolote humgusa moja kwa moja mmiliki wa jina la biashara
3. Huduma za kifedha
Kupata msaada wa huduma za kifedha kama mikopo kuendesha shughuli/biashara/miradi ni rahisi kupitia kampuni kwa sababu inasimama kama asasi yenye kujitegemea LAKINI katika jina la biashara unakopa binafsi hivyo kuna ugumu au kuna kuwa na kiwango cha msaada wa kifedha
4. Gharama za uendeshaji
Kampuni ina gharama mbalimbali za uendeshaji. Hii inatokana na kuwa na mfumo kamili wa kiutendaji ambao utahitaji kuwa na watendaji wengi kadiri inavyozidi kukua LAKINI jina la biashara ina maana waweza kila jambo kusimamia wewe binafsi
5. Uwasilishaji wa mahesabu
Kampuni inawajibika kuwasilisha mahesabu yaliyokaguliwa na mkaguzi wa hesabu kwa taasisi mbali mbali kama vile TRA katika kulipa kodi nk LAKINI jina la biashara unakadiriwa katika gharama kama kodi nk
6. Uwezekano wa kuendelea kwa kampuni kuwepo katika shughuki zake ni mkubwa hata mmiliki/wamiliki wakifa kutokana na muundo na asili ya utendaji kazi wake LAKINI jina la biashara kuna uwezekano wa kufa kwa biashara baada ya mmiliki kufa kutokana na kila jambo kuwa la mmiliki tu
7. Tenda, kazi nk
Kampuni ina nafasi kubwa sana ya kupata mfano tenda au kazi inapoomba kama kampuni kuliko jina la biashara. Hii inatokana na masuala kama umiliki katika mtazamo wa kisheria nk
Hizi ni baadhi tu.