Naomba kuwauliza wajumbe wenye uelewa au uzoefu wa kusajili kampuni humu ndani suala hili. Hivi hizi kampuni zinazotoa huduma ya kufanya uchunguzi (Research) zipo kwenye aina gani ya kampuni?
Je, hatua za kufuata kusajili kampuni za aina hiyo tajwa hapo juu zinafanana na usajili wa makampuni tofauti na hayo?
Pia, napenda kuuliza, je nikifungua kampuni ya kufanya utafiti wateja wangu wakuu ni akina nani hasa kati ya serikali na taasisi binafsi? Je hali ya soko la utoaji huduma za kufanya uchunguzi kwa Tanzania lipoje?
Mwisho kwa sasa, naomba kuuliza; inawezekana kusajili kampuni ya kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na kampuni nyingine kama sehemu ya kupata uzoefu maana najua mwanzo ni mgumu.
Ahsanteni.