Vipimo: anza na karangu nusu na sukari nusu,iliki km punje Saba HV zinatosha kuleta kaharufu kazuri. kwanza zitoe uchafu karanga zako pili zikaange bila mafuta mpaka uzione zmekuwa kavu...zitoe maganda zote! ukimaliza zitwange sanaa kwenye kinu mpaka uone zinatoa mafuta! Baada ya hapo chukua maji kiasi cha nusu lita bandika jikoni, tia na ile iliki (uitwange). Acha sukar ichemkeeeee sanaaaa impaka iive...utajuaje km imeiva? ukiishika na vidole viwili utaona inanata! au ukichukua mwiko ukifanya km unairudishia kwenye sufuria utaiona ni nzito unavutana! hapo utatia zile karanga zako ulizotwanga! utakorogaa bila kuachia mkono! ukiicha sekunde tu unaungua chini! utakoroga mpaka utakapoona imekuwa nzito utaimimina kwenye sinia ulilolipaka mafuta kidogo! utaicha mpaka ipoepoe utaanza kukata na kisu kikali shape unayopenda! ukipika mara kwa mara utagundua utakapokosea! pika nusu nusu mpaka utakapokuwa mtaalam utapika nyingi..kila la kheri