Jinsi ya kutengeneza kashata

Jinsi ya kutengeneza kashata

Aisee Tam kweli hizi mkuu.
Maana Dar zipo kibao watu wanauza,za rangi Nyekundu na zingine Kijani
Kipande Mia tu unajidai.
 
Ni kwamba unachukua Unga wa Ubuyu,unachanganya na Rangi uipendayo,hizi rangi zinauzwa maduka tele hadi mitaani na ni kama rangi zile tu za kwenye Ice cream za mtaani za mia mia,then unaweka Sukari na kuuchanganya Unga wa Ubuyu hadi sukari iwe kwenye kiwango cha ladha unayoitaka.

Unaweka Maji kidogo kulingana na Kiwango cha uwiano wa Unga kama ulivyofanya kwenye michanganyo hapo juu.

Kisha unaupiga kama vile unakanda matofali vile,kwa muda kiasi hadi uwe Mgum na kukaza,then ukiisha kaza ndio unaanza kukata vipande unavyotaka kwa utulivu.
Unaweza ku add na other Spices

Ila kama upo Dar,
Neda Kule kwa Somanga,ni maarufu sana Jiji la Dar kwa biashara hii.
Ni Babu wa Kisomali yupo pale Magomeni kama njia ya kwenda Tandale Uzuri,ukimaiza kituo cha Fundikira kifuatacho ndio kwa Somanga,hata mtoto mdogo ukimuambia atakupeleka.
Anauza Ubuyu wa Vanila,na pia anauza Unga wa ubuyu ambao tayari una rangi.
Wewe unanunua unachekecha,unatoa mizizi,then unaweka Sukari na kuanza kuupiga ili ujikaze na kisha kutaka
 

Attachments

  • 1438096223068.jpg
    1438096223068.jpg
    64.6 KB · Views: 418
Last edited by a moderator:
Hii niliitengeneza ikatokea vizuri mpendwa, ahsante kwa ujuzi. Naomba utuelekeze kuandaa hichi kitu kinaitwa fagi inshaallah,
 
hi wana jf,nimejaribu kutengeneza kashata ya ubuyu ikawa ngumu sana.
msaada kwa anaefahamu namna ya kuiandaa iwe lain
 
Habari zenu wapendwa mwenye kujua kupika kashata za ufuta naomba anielekeze pls
 
Jinsi ya kuandaa
. Osha vizuri ufuta kisha anika juani ukauke
. Weka sufuria jikoni, kisha weka sukari ndani ya sufuria, acha sukari ichemke hadi iwe kama inayeyuka
. Mimina ufuta ndani ya hiyo sukari, vichanganye hadi vichanganyikane kabisa
. Unatoa kidogo kidogo unatengeza shape ya duara kwa kuvibumba mkononi
Kashata zipo ready
 
Salamu zenu wakuu,

Naomba kuuliza mwenye ujuzi wowote wa kutengeneza kashata za unga wa ubuyu anisaidie ili nianzishe ujasiriamali.

Natanguliza heshima.
 
Naombeni mnielekeze jinsi ya kutengeneza kashata na vitu vinavyohitajika katika utengenezaji.
 
Back
Top Bottom