Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na ukioga usioge na sabuni maana vitundu vya vinyweleo vinakua havija funga so soap contain chemical so huleta muwasho baada ya kuogaNi vizuri ukatulia kidogo kabla ya kuoga.
Nini tofauti ya kujogg na kuruka kambaKubox siyo cardio, ile mtu huifanya baada ya kufanya mazoezi ya kukimbia na kuruka kamba (yaani baada ya kutengeneza pumzi). Ndiyo maana kama mtu ambaye hana msingi wa pumzi akipiga punching bag ngumi nne, aki-bob na ku-weave mara tatu anatoka jasho na pumzi zinampaa.
Kwa uzoefu wangu bado kujogg ni better cardio, ili kuipata the best inabidi uunganishe hizo cardio kutengeneza kitu kimoja.
Fanya crunches, sit ups, na kama una roller itumie.
Kwa kua unaanza.
Sit ups, Roller na Crunches fanya seti nne, kila seti fanya mara kumi.
Yapo mazoezi mengi ya tumbo naamini kuna wadau watakutajia ila anzia na hayo ukiwa advanced tutazidi kuongeza spices.
Hua unaifanyaje mkuu? Mimi nimeifanya tangu naanza mazoezi haijawahi kuniumiza na kuna watu nawajua haijawahi kuwaumiza.Roller sio nzuri,inaumiza mgongo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mh mkuu siyo kweli, kama maisha yako hayahusishi kupiga ngumi nako kuja ni mara chache. Mcheki Magufuli.
Ili misuli itanuke inabidi kuongeza reps na set kama ulivyosema. ILA pia kwa wale wanaoenda gym wanatambua iliku gain muscle Ina bidi kuongeza uzito unaobeba. Inashauriwa ubebe mzigo mgongoni wakati unapiga push up ukiwa umeshazoea ili kujenga kifua.Inakuaje wadau?
Nimeanza mazoezi ya kunyanyua uzito (I hate saying vyuma) mwaka 2013. Katika mazoezi hua tunasema majukumu ndiyo mchawi wa mazoezi, hivyo majukumu ya chuo yalikua yakinifanya nisiingie gym vile ninavyotaka iwe.
Wakati mwingine unajikuta unakosa pesa ya kuingia gym hivyo unajikuta huna option zaidi ya kukaa nyumbani ukiangalia ulivyoviingiza kwa wiki sita vikipukutika.
Lakini kwa muda nimekua nikitumia njia ambayo inanifanya kuubakisha mwili kwa kuujaza na kuukata.
Best of all, hili zoezi unaweza ukafanya popote na ndani ya dakika 45 (kutegemea na unavyotaka kua challenged).
Ili kuyafikia malengo ya hapo inabidi tufanye haya mazoezi kwa kutumia mtindo unaoitwa Tabata Protocol.
Zoezi tutakalolifanya litakua ni push ups (pushapu).
Na kanuni yetu itakua;
Zoezi moja litajumuisha seti nne.
Seti moja itajumuisha reps 20.
Kupumzika kati ya seti na seti ni sekunde 10.
Kupumzika kati ya zoezi moja na jingine ni dakika moja.
Anza na Pushap za Kawaida.
Hii ni ile aina ya pushap ambayo watu wengi wameizoea. Kama alizopiga Magufuli ila wewe usikunje ngumi.
View attachment 462249
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.
Hapo tunakua tumemaliza zoezi moja tunaenda jingine.
Pushap za miguu ikiwa imeinuka.
Mimi hua naweka miguu kitandani, unaweza ukaiweka kwenye stuli, jiwe au hata ndoo ukiigeuza juu chini. Pale daraja la Manzese miguu hua inawekwa kwenye ngazi.
View attachment 462252
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.
Hapo tunakua tumemaliza zoezi la pili, tunaenda jingine.
Tunakuja na Spartan Pushap.
Mikono yako inatakiwa ipishane, mmoja uwe mbele kushinda mwingine. Lakini ukiwa unaenda juu mkono uliokua mbele utaurudisha nyuma na uliokua nyuma unaupeleka mbele.
View attachment 462253
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.
Hapo tunakua tumemaliza zoezi la tatu tunaenda jingine.
Tunamalizia na Pushap za Magoti kugusa Chini.
Unaweka mikono kama unataka kupiga pushap alizopiga Magufuli, ila magoti yako yatakua yamegusa chini na usikunje ngumi kama Magufuli.
View attachment 462255
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.
Hapo tunakua tumemaliza zoezi letu.
NB.
-Utavuja sana jasho ndani ya dakika moja
-Kama hujawahi kufanya mazoezi, usifanye spartan pushap na hii ya magoti kugusa chini kwa sasa mpaka utakapozoea. Pia punguza idadi ya seti na reps, jiongezee na muda wa kupumzika.
-Natumia uzoefu na kujifunza kwa wengine, sijasomea, ushauri wangu siyo wa kidaktari.
-Comment workout yako tupate kujifunza.
Hakuna kitu kama hicho. Muscles haziwezi kujitengeneza pasipo a scheduled body exercises with balanced food.Mazoezi bila kula ni bure kabisa. Kuna vyakula ukila vizuri mtu anaweza fikiri unaenda gym hata kama huendi.
Yeah kaka nilijifunza katika kipind nipo university coz inaitwa principle of Heath and management kua ukitoka tiz oga without soap maana mwili pia huzalisha chemical unapopiga tiz so ile chemical inatoka kwa njia ya jasho so ukioga na sabuni ilhali sabuni ina chemical unakua unajaza chemical juu ya chemical ndio yale unaanza jikuna kuna then vimiwasho mara tuvipele due to hiz factor kuna wengine husema zile protex soap ni salama ndio wengi huzitumia but according to this education ni bora ukaoga hivihivi but maji yawe safi tu.Ni knowledge mpya kwangu asante mkuu