Jinsi ya kutengeneza siagi ya karanga

Jinsi ya kutengeneza siagi ya karanga

JINSI YA KUTENGENEZA SIAGI YA KARANGA-PEANUT BUTTER





Utangulizi:

Siagi ya karanga ni uji/laini mzito uliotengenezwa kutokana na karanga zilizokaangwa na kusagwa. Siagi hii inaweza kuongezwa utamu na vitamini. Siagi ya karanga inatumika kwenye mkate, kupikia na kuchanganya na vyakula mbalimbali.

Viambaupishi: Karanga, mafuta yasiyoganda, chumvi, sukari ‘stabilizer’ Lecithin

Vifaa: Mashine ya kusagia, sufuria, jiko la mkaa, mwiko, mzani wa kupimia.

Hatua za uzalishaji:

1. Malighafi
Chagua karanga zilizokomaa, kavu na zenye ukubwa unaofanana. Angalia zisiwe na ukungu kama vile “Aspergillus flavus”. Karanga ziwe na mafuta asilimia

2. Kusafisha na kuchagua
Peta karanga kutoa uchafu na takataka zilizomo- toa karanga mbovu na zile zilizosinyaa au kushambuliwa wadudu/ chembechembe

3. Kaanga.
Kaanga kwa uanglifu kwenye joto la kutosha ili karanga ziive bila kuungua, ha tua hii inazipa karanga rangi ya kikahawia kidogo na kuleta harufu nzuri.

4. Toa ganda

Toa maganda kwenye karanga na kutoa zile zilizoungua
.
5. Saga
Saga karanga mpaka kufikia ulaini unaotakiwa.

6. Changanya
Chemsha siagi kufikia joto la 80[SUP]o[/SUP] [SUB]C[/SUB] – 90[SUP]o [/SUP][SUB]C[/SUB][SUB],[/SUB]changanya na mafuta sukari chumvi asilimiana “stablizer” NB stablizer inawezkuongezwa wakati wa kusaga karanga (wakati wa kurudia).

7. Jaza

Kwenye chupa safi zilizochemshwa na kukaushwa. Ijazwe huku ikikorogwa ili kutoa hewa. Acha nafasi kidogo juu na funga kabisa hewa isipite. Unaweza ukaweka mafuta sehemu ya juu kwa kiasi kidogo ili kuzuia hewa isiingie kwenye siagi yako.

Imeandaliwa na Mtaalamu wetu wa Chakula. chanzo.ONE CLICK Habari: JINSI YA KUTENGENEZA SIAGI YA KARANGA-PEANUT BUTTER
Aksante kwa kutupa elimu ya bure
 
Mbona easy. Take this simple stapes

1. Chukua karanga zile za mafuta ( maarufu kama karanga za lishe) zilizomenywa tayari
2. Zichambue vizuri na chagua zenye ukubwa sawa
3. Kama unataka ziwe na ladha ya chumvi, basi zichanganye na maji yenye chumvi kiasi (kisha zianike juani zikauke)
4. Chukua sufuria kisha tia mchanga ndani yake. Pasha kwenye jiko (mi huwa natumia jiko la mkaa-for best results)
5. Mchanga ukishapata joto kiasi, weka karanga zako kisha rusharusha sufuria ili karanga zijichanganye na mchanga wa moto. ANGALIZO TUMIA MOTO WENYE JOTO LA WASTANI, ILI ZISIUNGUE
6 Endelea kuzigeuza kwa kurusharusha sufuria (AFTER 30 SECONDS TO 1 MINUTE), mpaka utakapoona karanga zimeanza kuiva.
N:B Karanga zikianza kuiva utasikia zinanukia, na hata ukipukucha punje utaona zinamenyeka kutoka katika layer yake kiurahisi
7. Epua sufuria kisha mwaga mchanganyiko wa karanga na mchanga katika sakafu au sinia
8. Zitoe karanga zako ziweke kwenye ungo.
9. Zisugue kwenye ungo kutoa layer yake, kisha pembua maganda (layers) na zibaki karanga tu
10. Saga karanga zako kwenye mashine ya kusagia karanga(ina fanana na ile ya kusagia nyama au viungo vya sambusa) mpaka karanga zako ziwe laini kabisa mithili ya blueband.

Weka katika chombo safi kwa ajili ya matumizi yako. Waweza kutumia kama bread spread maana huwa ni laini sana. Pia waweza kutumia kama kiungo cha mboga za majani. (MI HUWA NATUMIA PIA KWA MAPISHI YA SAMAKI WAKAVU/WALIOKAANGWA AU DAGAA WALIOKAANGWA) Inanoga pia

N:B Mchanganyiko huo hukaa muda mrefu pasipo kuharibika au kuchacha. Pia kadiri mchanganyiko unavyokaa hujichuja mafuta, ambayo pia ni kiungo kizuri kwa mboga hasa za majani.

ENJOY
 
Back
Top Bottom