Jinsi ya kutengeneza video za cartoons

Alphaking2023

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
2,092
Reaction score
2,123
Wasalaam,
Napenda kujifunza kutengeneza animation za cartoon huwa ninakuwa na ideas za scripts nyingi sana Ila sina sehemu za kuziwasilisha kama inavyotakiwa naomba wenye ujuzi na hizi animated cartoon atupe ujuzi hapa na sisi tuweze kutengeneza.
Nawasilisha
 
Ukiwapata nistue ninazo ideas nyingi mpk ubongo umejaa..!
 
Swali: una laptop au computer hapo kwako?
 
Swali lako ni pana sana labda umejaribu kufanya nini hadi sasa? Umewahi kuandika hizo idea zako katika script? Unajua kuchora na kutengeneza characters, na kama unajua umeshawahi kuchora hata kwenye karatasi. Unajua kutumia software za kuchora kwenye kompyuta kama Photoshop?

Kuna technique nyingi za kutengeneza animated cartoon, ikiwemo kuchora kwa mkono kila fremu kama katuni za zamani za Disney, Stop-motion animation ambazo unamsogeza mdoli kisha unampiga picha kisha unaziunga picha itokee video, kutumia 3D software kama Blender kutengeneza cartoon za 3d au hata za 2d, kutumia software za animation kama Flash, kwa kuanza unaweza ukaangalia software kama OpenToonz kupata idea.


 
Nimeangalia hizo video na ndo ujuzi ninaoutaka huo hasa hii video ya chini kwenye animation namba tano iko poa zaidi mi sio mtaalamu wa kuchora kiukweli kipaji hicho sina labda kama kuna njia zingine za kutengeneza animation bila kuchora ndo itakuwa nzuri zaidi kwangu
 
Laptop ipo
Sasa kama laptop unayo na internet connection ndo hii WHAT ARE YOU WAITING FOR? mi nadhani mdau hapo juu kakupa muongozo mzuri sana wa nini cha kufanya kwanza au wapi pa kuanzia ikiwemo na software zinazohitajika kama uko SERIOUZ i hope ushaanza kuzifanyia kazi!
 
mkuu mimi najua kuchora kwa mkono. Tena kwa katuni nilishachoraga hadi kwenye magazeti fulani japo kwa muda mfupi wa mwaka mmoja tu. Je, kwangu kuna urahisi wa kutengeneza animation?. Na je zile za 3D nazo zinahitaji uchoraji???

mimi pia nina ideas kibao aisee but tatizo tools tu ndo zinanivunjaga moyo. Maana niliambiwa shughuli hii inajitaji computer iliyoshiba eti
 
wadau mko poa mimi nachora na kutengeneza vikatuni aina zote 3D na 2D kama unahitaji kufahamu zaidi nitafute kwa namba hizi 0769412198
 
Nafurahi sana kuona vijana Wanajikita kujua mambo lakini pia nasikitika kuona kwamba hakuna expert wa kutoa msaada Mimi kwa uelewa wangu sijawai publish cartoon mtandaoni lakini nilitengeneza chache bahati mbaya zilipotea kwenye computer niliyokuwa natumia any way fuata maelekezo haya
Kutengeneza cartoon kunaitaji Vida vingi vya muhimu kama computer,tablets na ujuzi wa namna ya kutumia software maalum inategemeana na aina ya cartoon unayo taka.
Kwa 2D cartoon kuchora uwezi kimbia ni lazima ufahamu mara nyingi tunatumia tablet maalum ya kucholea google utaziona au ntakuletea baadae hapa jukwaani
Hapa utachora character kwa kila pose unayotaka ionekane then kwa kutumia software kama adobe illustrator utadesign ili kile ulicho chora kwa mkono au tablet uwa na format tunaita raster Image kiwe na format ya vector Image kwa ajili ya kufanya animations
Hapa utatumia software kwa ajili ya 2D mfano adobe Flash sasa hivi inaitwa adobe animate kama sikosei pia kuna software kama anime studio ,toon boom n. K
Kwa 3D
Kuchora pia ni lazima ujue la sivyo utafanya Project ichukue muda mlefu kutengeneza picha kwani unatakiwa uwe na ides inayoonekana hapa unaitaji ujuzi wa kutumia 3d software napendekeza jifunze blender software kwanza alafu njoo ujifunze software inaitwa 3d lightwave ila napendekeza utumie maya au 3dsmax software
Mimi zote nilijifunza ila niliamua kutumia blender na cinema4D
Kama unaswali uliza pia kuna jamaa ubungo river side anaitwa fred adam mtafute kama uko dsm kama uko mbali tafuta torrent course za animation za jamaa anaitwa george maestri amefundisha software zote zilizotrend kwenye soko la 3danimations
Kama Maya, 3dsmax, blender, cinema 4d n. K
Au nunua cd ya cgmasters ukiwa mtaalamu wa torrent client utaipata kwa bando la internet
 
Swali lako pana Ila somehow naweza kufaham unacho taka kujifunza(Animation)
Kabla hujaanza unapaswa kujiuliza maswali haya mawili
1.Nianzie wapi?
2.Ni software gan sahihi kwa beginner kama mm?

A) Nianzie wapi
Animation kimsingi ni pana kwa maana ndani yake kuna categorie Kubwa zaidi ya nne I.e unaweza kukaa upande wa Games, VR, 3D animation nk
Kwa kuchagua kimoja kati ya hivyo mfano 3D animation utapata nafasi ya Kuenda Level ya pili ambayo Ni
"Fundamentals of 3D animation" ambapo ndani ya hizo Fundamentals utakutana na Fundamentals nne(4):-
1)Modeling
2)Texturing
3)Lighting
4)Rendering
Zaidi ya yote. Ukimaliza hapo utalizimika kuzifahamu "Principals of 3D animation ambazo zipo 12.

B) Ni software gani sahihi kwa beginner?
Zipo Software nyingi mno ambazo hutumiwa na studio kubwa na animators wakubwa wakubwa kuacha na Pixer ambao wao wanatumia software Yao wenyewe ambayo haipatikani popote zaidi ya pale pixer na haiuzwi popote pale.

Unapo kuja katika swala la Software ni lazima uzingatie mambo haya
1)Price
2)Urahisi wa Kutumika
3)Ufanisi

Kipekee ningependa uanze na BLENDER. Sio kwamba mm nilianza na BLENDER eti nikuambie uanze na BLENDER bali Nina sababu kadhaa ambazo zitajikita katika Price(Budjet), Urahisi wa Utumiaji wa hiyo software na Ufanisi. Sasa ukija katika swala la Price, BLENDER inapatikana BURE kabisa tofauti na MAYA ambayo ni ghali $2700/Year, BLENDER ni rahisi kujifunza na Kukuwezesha wa kufanya mambo yako, Ufanisi wa BLENDER ni wa hali ya Juu Siku zote.

Note: Katika kujifunza 3D animation kabla hujaanza kutengeneza Projects zako, ni lazima kwanza uisome 80/20 Rule.

MY TAKE: 3D animation sio rahisi kujifunza na kufanikiwa kwa haraka maana ni jambo litakalo kuchukua muda wako mwingi mno Lakini "Kwakua teyari Wapo walio fanikiwa katika hilo, basi utajifunza kutoka kwao na kufanikiwa" ni sector yenye Pesa ndefu mno maana mshahara wa 3D animator Kwa wenzetu huko nje ni not less than $64,000 .

Ni matumani yangu nimeweza angalao kukupa mwanga.
[HASHTAG]#mtokambali[/HASHTAG]
 
Asante umenipa mwanga ila hiyo 80/20 rule unayoizungumzia ndo ile ya kusema 20% ya unayofanya yanachangia 80% ya matokeo au hyo ni rule nyingne?
 
T
Tafuta software by the name of Maya. It is a professional 3-Dimensional software that is globally recognized. Thereafter, tafuta tutorials on youtube and other sites to perfect your skills.
 
T

Tafuta software by the name of Maya. It is a professional 3-Dimensional software that is globally recognized. Thereafter, tafuta tutorials on youtube and other sites to perfect your skills.
Shukran kwa mchango wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…