Wasalaam,
Napenda kujifunza kutengeneza animation za cartoon huwa ninakuwa na ideas za scripts nyingi sana Ila sina sehemu za kuziwasilisha kama inavyotakiwa naomba wenye ujuzi na hizi animated cartoon atupe ujuzi hapa na sisi tuweze kutengeneza.
Nawasilisha
Swali lako pana Ila somehow naweza kufaham unacho taka kujifunza(Animation)
Kabla hujaanza unapaswa kujiuliza maswali haya mawili
1.Nianzie wapi?
2.Ni software gan sahihi kwa beginner kama mm?
A) Nianzie wapi
Animation kimsingi ni pana kwa maana ndani yake kuna categorie Kubwa zaidi ya nne I.e unaweza kukaa upande wa Games, VR, 3D animation nk
Kwa kuchagua kimoja kati ya hivyo mfano 3D animation utapata nafasi ya Kuenda Level ya pili ambayo Ni
"Fundamentals of 3D animation" ambapo ndani ya hizo Fundamentals utakutana na Fundamentals nne(4):-
1)Modeling
2)Texturing
3)Lighting
4)Rendering
Zaidi ya yote. Ukimaliza hapo utalizimika kuzifahamu "Principals of 3D animation ambazo zipo 12.
B) Ni software gani sahihi kwa beginner?
Zipo Software nyingi mno ambazo hutumiwa na studio kubwa na animators wakubwa wakubwa kuacha na Pixer ambao wao wanatumia software Yao wenyewe ambayo haipatikani popote zaidi ya pale pixer na haiuzwi popote pale.
Unapo kuja katika swala la Software ni lazima uzingatie mambo haya
1)Price
2)Urahisi wa Kutumika
3)Ufanisi
Kipekee ningependa uanze na BLENDER. Sio kwamba mm nilianza na BLENDER eti nikuambie uanze na BLENDER bali Nina sababu kadhaa ambazo zitajikita katika Price(Budjet), Urahisi wa Utumiaji wa hiyo software na Ufanisi. Sasa ukija katika swala la Price, BLENDER inapatikana BURE kabisa tofauti na MAYA ambayo ni ghali $2700/Year, BLENDER ni rahisi kujifunza na Kukuwezesha wa kufanya mambo yako, Ufanisi wa BLENDER ni wa hali ya Juu Siku zote.
Note: Katika kujifunza 3D animation kabla hujaanza kutengeneza Projects zako, ni lazima kwanza uisome 80/20 Rule.
MY TAKE: 3D animation sio rahisi kujifunza na kufanikiwa kwa haraka maana ni jambo litakalo kuchukua muda wako mwingi mno Lakini "Kwakua teyari Wapo walio fanikiwa katika hilo, basi utajifunza kutoka kwao na kufanikiwa" ni sector yenye Pesa ndefu mno maana mshahara wa 3D animator Kwa wenzetu huko nje ni not less than $64,000 .
Ni matumani yangu nimeweza angalao kukupa mwanga.
[HASHTAG]#mtokambali[/HASHTAG]