Jinsi ya kutengeneza website(tovuti) bure ya kiofisi (acha kulipia leo)

Jinsi ya kutengeneza website(tovuti) bure ya kiofisi (acha kulipia leo)

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
31,559
Reaction score
42,179
Habari WanaJF,

Nimeandaa hii tutorial kuwasaidia watu wenye ofisi ndogo ndogo na watu binafsi ambao wanataka kuwa na website kwa ajili ya biashara zao au matumizi binafsi lakini kutokana na ukosefu wa hela au uelewa kuhusu lugha za kucode website wameshindwa kumiliki.

Fuata hizi process kwa umakini na utaweza kufungua website.

IDEA (wazo)
Ili uwe na website lazima kwanza uwe na wazo lako kama ni mfanyabiashara ina maana wazo lako ni hiyo biashara na website yako nayo itahusu hiyo biashara. Kama ni mtu binafsi nakushauri wazo lako liwe unique na usiige ige watu utaishia pabaya.

KUTENGENEZA WEBSITE
Hapa kuna aina mbili za utengenezaji rahisi utaangalia aina itakayokupendeza nazo ni kutengeneza online au offline

-offline website building
Kwa sababu hujui language ya kukodi website utahitaji msaada wa software. hizi software zipo nyingi ila ntataja maarufu zaidi ambazo nimeshazitumia ili iwe rahisi zaidi kwangu kukuelekeza sehemu utakayokwama. Na nimezigawanya sehemu mbili za website za kawaida na flash website.

(a) software ya website za kawaida WEBSITE X5 EVOLUTION
boxshotev9_en_200.png

Hii kwa muono wangu ni software rahisi zaidi kwani unachagua design na kuadd picha na maneno tu website yako inakua tayari inaeleweka kiasi kwamba hata beginer ataweza kuitumia. Ukimaliza kutengeneza website utasave hio website kama file. Kama utapata tatizo utanijulisha
Link yao ni hii hapa

Free Demo Software ? Download WebSite X5 ? make a website - WebSite X5

(b)software ya flash website A4 DESK PRO
a4deskpro-flash-website-builder-trans.png


Flash website ni za kisasa kidogo kuliko za kawaida na pia ili kuvisit flash website inabidi flash player iwe installed katika device. Simu ambazo sio smart phone hazisupport flash website. Hii mara nyingi sio nzuri kua official website ya business ila ni nzuri kwa mambo ya entertainment.

Utadownload hii software na kuchagua template na ku add text na picha hamna programing language. Nayo ukimaliza kutengeneza website utasave file lake.


Kudownload hii software click link ifuatayo
Download Website Building Software

Zipo software nyengine kwa faida yako mwenyewe utaenda kuzitest
-dreamwaver
-frontpage
-netfussion
-web studio
-n.k

HOSTING WEBSITE
Sasa tumemaliza kutengeneza website now itabidi tuihost online ili ionekane. Katika step hii ndio utahitajika ku upload lile file la website ulilopata baada ya kumaliza kutengeneza.

Hapa ntataja hosting chache ambazo ni za bureee.

servers free best hosting
Why nasema hawa jamaa ni best? Watakupa space ya 10 gb kueka mafile yako na bandwitch ya gb 100, huwa hawaban ovyo account na wapo fast.

Cha kwanza fungua acount chagua subdomain halafu nenda cpanel yako utaona link imeandikwa import website click hapo then upload ile website yako utakua umemaliza kazi.
Link yake

Servers free – free web hosting servers, servers for free, free server

other hosting
Kutokana process za host nyingi zinafanana ntazimention tu free hosting

Free Web Hosting with cPanel, PHP, and no Ads
Free Web Hosting - Linux, PHP, MySQL, No Ads/Banners by FreeHostia.
Free Web Hosting with PHP, MySQL and cPanel, No Ads
Free Hosting, Paid Hosting, Reseller Services & VPS Servers : Byet Internet
Webs - Make a free website, get free hosting

DOMAIN
Ok tushatengeneza website lakini ina subdomain tu haina domain kamili inabidi tutafute jina zuri kwa ajili ya website yetu so hapa lazima tutengeneze domain

Kabla sjataja website ya domain inabidi kwanza ujue tutorial namna ya kupark domain

Cha kwanza utaenda kwenye host yako sehemu ya domain then uchukue dns zao. Mfano nahost website seversfree.com basi dns itakua namna hii

ns1.serversfree.com
ns2.serversfree.com

Ukishazipata unaenda website ya kutengeneza domain then unregister unachagua jina unalopenda halafu unachagua domain by dns then utaeka dns zako

Baada ya hapo unarudi kwa host wako kupark hio domain
Nb: inaweza chukua hadi masaa 24 kwa domain kua tayari so kua mvumilivu

website za kutengenezea domain
dot.tk best domain
Hii ndo top level domain pekee inayokubalika google ambayo ni free kuregister just nenda link hii
Dot TK - Free Domains for All

Website nyengine za domain ni
uni.cc

co.nr
afraid.org
net.tc
net.tf
co.cc
co.tv

Kama utapata tatizo lolote usisite kupost hapa
 
Ina maana kama nina domain mie na register na kupata host bureeeeeeeeeeeeeeeee...?
 
Ina maana kama nina domain mie na register na kupata host bureeeeeeeeeeeeeeeee...?

Yah bio ni bure sema si free hosting zote zinakua nzuri so kama ushauri tu ni vizuri u google details za hio hosting kujua watu walioshatumia wanasemaje.

Ila serversfree naitumia mda mrefu iko poa
 
Yah bio ni bure sema si free hosting zote zinakua nzuri so kama ushauri tu ni vizuri u google details za hio hosting kujua watu walioshatumia wanasemaje.

Ila serversfree naitumia mda mrefu iko poa

Haina noma ngoja nihost domain yangu hapo nione mziki wake mkuu.
 
Shukrani sana kwa darasa zuri. Mungu akubari!
Swali langu: after completing all steps mentioned above..will the website be searchable by google?
 
Shukrani sana kwa darasa zuri. Mungu akubari!
Swali langu: after completing all steps mentioned above..will the website be searchable by google?

Thats easy ukimaliza kutengeneza website ikishakua online tengeneza acount ya google halafu uta add url katika google webmaster tools link yake hii hapa

http://google.com/addurl

Kuna hosting wengine automatic website yako inakua listed google ila sishauri hivyo kwa sababu utakapokua na acount ya google webmaster utajua ni keywords gani inakuletea visitors wengi, ni vipi ufanye website yako iwe visible sana na mengine mengi
 
Thats easy ukimaliza kutengeneza website ikishakua online tengeneza acount ya google halafu uta add url katika google webmaster tools link yake hii hapa

http://google.com/addurl

Kuna hosting wengine automatic website yako inakua listed google ila sishauri hivyo kwa sababu utakapokua na acount ya google webmaster utajua ni keywords gani inakuletea visitors wengi, ni vipi ufanye website yako iwe visible sana na mengine mengi

Shukrani mkuu.
 
Asnte kwa somo zuri my dear epert. Mungu akujalie kwa ukarimu,natumaini unafahamu fika uchoyo haulipi.Thanks to jamii forum too.Nimepata ujuzi bila malipo.
 
nice tuturial chief-mkwawa ila ukumbuke, its not bure as u trying to tell people, kuna vitu kama muda na gharama zingine eg: internet, creativity sio kila mtu ni creative kutengeneza kutengeneza eye catching website, kwa mtazamo wangu, let the professional stuffs be done by professionals, ila kama ni personal pages, blogs, etc poa mtu anaweza fanya mwenyewe

most of webhosts, wana online web builders, unafanya look n feel thing, inakuruhusu kutengeza simple html pages kama zamani kwenye ms frontpage, au publisher,

all in all concept ya FREE as free hakuna kitu kama hicho hapa duniani, haijawai kutokea na haitatokea
 
Last edited by a moderator:
Vp kuhusu kufupisha urefu wa domain nane kwenye hizo free hosting??

Sjakuelewa kufupisha kivipi lakini ntakujibu kwa ujumla

kufupisha kwa top level domain
Ninaposema top level domain nina maanisha domain maarufu kama za .com .net na .org

always ni za kulipia na bei average ni elf 20 japo unaweza ipata rahisi hadi sh elf 10 au chini ya hapo

Na zinakubali kwa free hosting utanunua domain yako then unakuja kuipaki kwenye free hosting.

Ni vizuri pia sometime ukanunua domain kwa wale wanaokupa hosting ya bure (kama sio mhuni huni).

kufupisha domain kwa huduma maarufu kama shorten url

Hapa unaeka domain au page yoyote ambayo ni ndefu then wanaiconvert kuja fupi zipo website za mfano huu

-jamiiforums.com
-Bit.ly

Ukiconvert website yako inakuja hivi

-jamiiforums.com/qwerty
-bit.ly/qwerty

Hope umenpata
 
kuna mtu kaona mwenzie katoa somo free anaanza kumkosoa,,,,,,mkuu chief mkwawa big up hata kama kunamalipo siwez kujali kwa sababu hata kuanza nilikua sijui sasa hiv angalau kuna matumain flan yapo...thanks mkuu
 
Back
Top Bottom